Dec 20, 2013

Wasichana wa Kisyria wauzwa nchini Algeria

Duru za habari zimefichua habari ya kuweko mitandao ya magendo ya binaadamu nchini Syria  na Algeria ambayo hujishughulisha na kuwanunua na kuwauza wasichana wa Kisyria  na kuwapeleka nchini  Algeria. 

Gazeti la Alfajr la nchini Algeria, limefichua juu ya kuweko habari ya mabinti wa Kisyria wanaopelekwa nchini Algeria kwa lengo la kwenda kushughulishwa katika vitendo vya ufuska utumwa wa ngono na hata na kuuzwa kama bidhaa.
Hayo yamethibitishwa na maafisa wa usalama nchini Algeria wakati walipofanya mahojiano na gazeti hilo la Alfajr na kufichua jinai mpya dhidi ya binaadamu zinazofanywa na mitandao ya magendo ya binaadamu nchini Syria na Algeria. 

Katika mahojiano hayo maafisa wa usalama wa Algeria wamesisitiza kuwa, vita na machafuko ya ndani nchini Syria vimepelekea mabinti wa nchi hiyo ya Kiarabu kuwa bidhaa yenye thamani  kwa magenge ya magendo ya binadamu ambapo baadhi yao huuzwa kwa baadhi ya viongozi wa Algeria kama zinavyouzwa bidhaa nyingine. 

Kwa mujibu wa gazeti hilo mitandao hiyo ya magendo ya binaadamu, huwapatia pasi za kusafiria na visa za utalii wasichana na kuwapatia ahadi kemkemu za kuwatafutia kazi, lakini wasichana hao wanapofika Algeria hujikuta wakinasa katika mitego ya mitandao ya magendo ya binadamu.

0 comments:

Post a Comment