Dec 20, 2013

Rais Putin amuachia huru Khodorkovsky kiongozi aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali yake

Mikhail Borisovich Khodorkovsky akiwa kwenye moja ya jela aliyokuwa akishikiliwa
Mikhail Borisovich Khodorkovsky akiwa kwenye moja ya jela aliyokuwa akishikiliwa

Rais wa Urusi, Vladmir Putin ametia saini amri ya kuachiliwa huru kwa tajiri na mkosoaji mkubwa wa Serikali yake, Mikhail Khodorkovsky aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka kumi jela kwa makosa ya rushwa na ukwepaji kodi.

Akitoa tangazo lake, rais Putin amesema kuwa kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu anatangaza rasmi kutoa msamaha kabla ya muda wake kwa Khodorkovsky kuachiliwa huru kutoka gerezani bila ya kuendelea kutumikishwa zaidi akiwa huko.


Akizungumza kwenye mkutano wake na wanahabari hapo jana, rais Putin amesema kuwa amefikia uamuzi wa kumuachilia huru mwanaharakati huyo kwa kile alichodai kuwa ni ombi ambalo alilipokea kutoka kwa Khodorkovsky mwenyewe aliyesema mama yake anaumwa.

Khodorkovsky alikuwa tajiri wa kamouni ya mafuta ya Yukos na kampun yake ilituhumiwa pamoja na yeye kama mmiliki kukwepa kodi ya mabilioni ya fedha ambayo yangeweza kusaidia kukuza uchumi wa taifa hilo.

Khodorkovsky alitumia kiasi cha dola bilioni 20 za Marekani kusaidia kampeni za chama cha upinzani wakati wa uchaguzi wa mwaka 2003 saa chache kabla ya kukamatwa kwake.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa rais Putin anatafuta uungwaji mkono toka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo kwa kujaribu kuonesha anatawala taifa hilo kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu.

0 comments:

Post a Comment