Nchini Iraq milipuko mitatu imepelekea kuuawa Waislamu zaidi ya
35 wa madhehebu ya Shia waliokuwa safarini kwa ajili ya kufanya ziara
kwenye maeneo matakatifu na wengine wengi kuujeruhiwa katika maeneo ya
kusini mwa mji mkuu Baghdad.
Mlipuko wa kwanza ulitokea kwenye eneo la Dura ambako mtu mmoja alijilipua na kuua watu zaidi ya 20 huku wengine 40 wakijeruhiwa. Magaidi wengine wawili walijilipua kwa mabomu kwenye maeneo ya Yusifiyan na Latifiya na kuua kwa ujumla watu 16. Waislamu wengine 50 wamejeruhiwa.
Wahanga hao ni miongoni mwa maelfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaoelekea katika mji mtukufu wa Karbala nchini Iraq kwa ajili ya shughuli ya siku ya Arubaini ya Imam Hussein (A.S) mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW Jumatatu ijayo.
Mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Kishia kwa kawaida hufanywa na kuratibiwa na wafuasi wa kundi la al Qaida na mawahabi wenye misimamo mikali wanaofadhiliwa na nchi kama Saudi Arabia na Qatar.

0 comments:
Post a Comment