Viongozi wa Waislamu na Wakristo
huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wameungana ili kuzuia kuuliwa raia nchini
humo.
Askofu Mkuu Dieudonne Nzapalainga, na Imam Omar Kobine Layama,
kiongozi wa Waislamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameamua
kushikamana ili kuzuia kutokea mapigano zaidi kati ya wafuasi wa dini
hizo kufuatia kushadidi mapigano ya kikabila na kidini nchini humo
yaliyosababisha kuuliwa watu wengi.
Waasi wa zamani wa Seleka Jumapili wiki
hii walipigana na wanamgambo wa Kikristo na kushambulia makazi ya
kiongozi wa waasi hao wa zamani katika eneo la Galabadja na kufanikiwa
kulidhibiti eneo hilo, hatua ambayo imeibua hofu kwa wakazi wa eneo hilo
na kuwafanya wakimbilie makanisani kwa ajili ya kupata hifadhi
wakihofia kushadidi mapigano kati ya pande mbili hizo.
0 comments:
Post a Comment