Waziri wa Wakfu wa Syria amesema
kuwa nchi hiyo hatimaye itapata ushindi kwa kutegemea umoja na irada ya
wananchi katika kukabiliana na wapinzani wake.
Muhammad Abdulsatar al
Said Waziri wa Wakfu wa Syria amesisitiza juu ya udharura wa kuweko
umoja na mshikamano kati ya Waislamu na Wakristo ili kuweza kukabiliana
na makundi ya ukufurishaji ya Kiwahabi yanayolenga matukufu ya Kiislamu
na Kikristo.
Waziri wa Wakfu wa Syria ameyasema hayo jana katika Kanisa la Maryam huko Damascus mji mkuu wa Syria kwa mnasaba wa kusherehekea mwaka mpya wa 2014 Miladia.
Habari zinasema kuwa makundi ya kigaidi hivi karibuni yamezidisha jinai zao huko Syria baada ya kushindwa vibaya katika kukabiliana na jeshi na vikosi vya kiraia nchini humo.
Magaidi hao wanajaribu kutenda kila jinai zikiwemo za kuwaua ovyo raia wa Syria ili kuficha kushindwa kwao huko na jeshi la nchi hiyo
0 comments:
Post a Comment