Dec 25, 2013

Kundi la wanamgambo wa kislamu la Mujao nchini Mali laonekana kufifia

Kundi la wanamgambo wa kislamu la Mujao, kaskazini mwa Mali

Kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa kislamu katika jimbo la Gao, kaskazini mwa Mali, waliyodhibiti jimbo hilo katika mwaka wa 2012, amekamatwa baada ya makabiliano ya ufyatulianaji risasi na wanajeshi wa Mali, duru za kijeshi zimefahamisha.

Aliou Mahamar Touré, Kiongozi huyo wa zamani wa kislamu katika mji wa Gao, alikamatwa jana jumatatu na jeshi la Mali, baada ya makabiliano ya ufyatulianaji ya risasi, amesema muakilishi wa jeshi la Mali kaskazini mwa nchi.

“Alifyatua risasi kwa kutuzuwia tusimkamate, na sisi tulijaribu kujibu na tukamkamata, hakujeruhiwa na wakati huu iko njiani anaelekea Bamako kwa ulinzi mkali”, ameendelea kusema afisa huyo.


Kukamatwa kwa Aliou Mahamar Touré, ni pigo kubwa kwa wanamgambo wa kundi la Mujao linaloendesha harakati zake magharibi mwa Afrika.

Aliou Mahamar Touré, alikua nguzo kubwa ya kundi hilo,liliyodhibiti eneo la kaskazini mwa Mali katika mwaka 2012, kabla ya kutimuliwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waliyokua wakiongozwa na Ufaransa, mwaka 1 uliyopita.

Aliou Mahamar Touré, ni mzawa wa Gao, ambae alikua na cheo kikubwa katika kundi la wanamgambo wa kislamu.

Aliou Mahamar Touré,alikua akichukua adhabu kwa kuzingatia sheria za dini ya kislamu.

 Anatuhumiwa kumkata mikono mtu alietuhumiwa wizi, na kuwapiga bakora wanawake ambao walikua hawavai hijabu.

0 comments:

Post a Comment