Dec 24, 2013

Viongozi wa kislaam Afrika ya Kati watoa kauli yao na Askari wa Kifaransa auliwa.


somalimemo.net 
Makabiliano makali kati ya waislaam na wanajeshi walioivamia nchi ya Afrika ya kati imeibuka tena katika mji mkuu wa Bangwi.

Kwa uchache Maofisa watatu wa Wapiaganaji wa SILKA na Askari mmoja wa Jeshi la France wameuliwa kwenye mapambano makali yaliotokea mitaa ya kaskazini mwa mji wa Bangwi.


Wanajeshi wa France wanaoiunga mkono Wakristo walijaribu kuwanyaganya silaha makundi ya wapiganaji wa Kislaam,afisa mmoja wa Makundi ya wapiganaji wa Kislaam aliyezungumza na Televisheni ya Al Jazeera amesema wataendelea na mapambano yao dhidi ya wanajeshi wa France.

Upande mwingine mkutano wa dharura ulio wakutanisha wanasiasa,wazee wa kikoo na viongozi wa Kislaam nchini Afrika ya Kati wamekubaliana kusimama pamoja na waislaam.

"Viongozi wa Kundi la SILKA na Viongozi wa Kislaam wamekubaliana nchi ya Afrika ya Kati igawanywe pande mbili ya waislaam na Wakristo ili kuepusha maafa baada ya kutokea mauaji ya watu 600 kati makundi hizo mbili" alisema Mamado Al Qureyshi.

Maandamano makubwa yaliofanywa na waislaam yamefanyika mji mkuu wa nchi hiyo na watu walikuwa na mabango yaliokuwa na maneno,"hatuwataki wafaransa,Amani ndio! na Hatumtaki Mbabe wa Kivita Franso Olando" .

Serikali ya France ilishasema kuwa imewatuma wanajeshi wake zaidi ya 1600 ili kuwanyaganya silaha waislaam waliomwangusha Rais wa zamani Franso Bosise.

0 comments:

Post a Comment