Katika hali inayoonekana kuwa ni matumizi mabaya ya kodi za Wananchi ikiwemo Waislamu,Ofisi mbalimbali za Serikali zimepambwa kwa ajili ya Sikukuu ya X-MAS.
Hayo yamegundulika leo hii baada ya munira blog kufanya ziara katika taasisi mbalimbali za Serikali Jijini Dar es salaam.
Munira Blog ilipita katika Wizara kadhaa na kumalizia katika Ofisi ya TRA Ilala mtaa wa Kipata na kushuhudia Ofisi hizo zikiwa yamepambwa kwa maputo,vitambaa vya rangi mbalimbali huku taa (Disco light) zenye muziki zikiwaka.
Watu kadhaa walioongea na mwandishi wetu walionesha kutofurahia kodi za Watanzaia wote kutumika kwa ajili ya dini moja.
"Kimsingi siafiki jambo hili na nimekuwa nazungumza bayana kiasi kwamba baadhi ya wafanya kazi wenzangu wana nitafsiri mimi ni mdini,lakini hii si haki,iweje kuna pokuwa na X-MAS au Pasaka maofisi yanapambwa lakini kukiwa na Sikukuu za waumini wengine maofisi hayapambwi"alisikika mfanya kazi mmoja wa TRA iliyopo mtaa wa Kipata ambaye hakutaja jina lake.
Kwa upande wake dada aliyejitambulisha kwa jina la Joyce alisema japo yeye ni Muumuni wa Kikristo huwa anashangaa kuona Sikukuu za Waislamu hazipambwi katika maofisi mbalimbali lakini hajuwi undani wa hili.alisema.
Naye Bwana Rajab Mkazi wa magomeni,amesema "kwa kweli inauma kuona tunapuuzwa,tuna dharauriwa na watu wana fanya watakavyo,lakini yana mwisho na tusje kulaumiana"alisema bila ya kufafanua.
Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa Waislamu juu ya matumizi ya kibaguzi yanayo tokana na kodi za wananchi huku jamii ya dini moja ikionekana kubebwa katika kila sekta na Waislamu kupuuzwa.
Lakini kwa miaka yote hiyo Serikali hajawa na masikio ya kusikio vilio hivyo.
0 comments:
Post a Comment