Dec 24, 2013

Opresheni ya Westgate Al-Shabab iliwagharimu kiasi kidogo cha pesa".




somalimemo.net 
Vyanzo muhimu kutoka ndani ya Serikali ya Marekani kimebaini kuwa katika opresheni kubwa iliyofanyika katika Jengo la Kibiashara mjini Nairobi ambapo Kundi la Al-Shabab iliyo chini ya Kundi kubwa la Al-qaida walitumia kiasi cha fedha kisichozidi dola za Kimarekani elfu tano tu,kitendo hicho kinaweka wazi jinsi Makundi ya Kijihadi inavyoweza kutumia bajeti ndogo katika kutekeleza opresheni kubwa sehemu yeyote duniani.



Televisheni ya CNN iliyo na makao yake nchini Marekani imesema ikimnukuu afisa moja wa serikali ya Marekani kwa sharti la kutotajwa jina lake kuwa katika shambulio iliyofanyika Westgate na iliyoua watu zaidi ya 67 na mamia  kujeruhiwa na wengi wao wakiwa raia wa kigeni kutoka nchi za Magharibi,maandalizi ya opresheni hiyo na utekelezwaji wake umegharibu pesa ndogo sana,kama ilivyobainika vielelezo na vyanzo muhimu kutoka vitengo vya upelelezi ndani ya Serikali ya Marekani.


Vyanzo hivyo vinabainisha na kutaja Idadi ya wanaume waliotekeleza shambulio hilo siyo zaidi ya wanaume watano,ambao walikuwa na mabomu madogo madogo na silaha ndogo ndogo kama vile Ak47,na huko maelezo hayo yakigongana na maelezo iliyoitoa Serikali ya Kenya walioshambulio Westgate walikuwa watu 15 waliokuwa na silaha nzito nzito.


Kama inavyobaini vyanzo hivyo viliopatikana,kundi hilo lililofanya shambulio la Westgate walitumia mawasiliano ya kawaida sana ambayo walikuwa wakiwasiliana tangu kuanza kwa opresheni hiyo na mawasiliano yenyewe ilikuwa ni simu za Kiganjani walizokuwa wakitumia ndani ya Soko kubwa la Westgate.


Mashirika ya kipelelezi za nchi za Magharibi wamesema kiasi cha pesa kilichotumika kuishambulia westgate October mwaka huu ilikuwa kidogo sana ukilinganisha na mashambulio mengine makubwa iliyofanywa na Kundi la Al-qaida katika mataifambalimbali duniani.


Shambulio iliyofanyika nchini Marekani mwaka 2011 kilitumika kiasi cha Dola za Kimarekani laki tano,huko shambulio iliyofanyika Kisiwa cha Bali nchini Indonesia mwaka 2002 kiligharimu kiasi cha pesa za Kimarekani Dola elfu khamsini,pia upande wa shambulio iliyofanyika Madrid mwaka 2004 kiligharimu kiasi cha pesa za Kimarekani Dola Elf kumi na tano.


Chanzo cha Habari : CNN Arabic, http://arabic.cnn.com/world/

0 comments:

Post a Comment