Wakati baadhi ya waumini wa misikititi ya Tanzania wakiwaadhibu wezi wa viatu misikitini kwa kuwapa vipigo vikali,hali ni tofauti nchini Nigeria baada ya Mahakama moja jijini Abuja nchini humo iliyopo ndani ya Kado kutoa hukumu ya kifungo.
Hukumu hiyo ilitolewa Jumatano ya wiki hii kwa kijana Isah Abdullahi,baada ya kumuhukumu kifungo cha miezi minne jela mara baada ya kupatikana na hatia ya kuiba viatu pea saba msikitini.
Abdullahi toka kijiji cha Utako, Abuja, alikamatwa na polisi wakati akiwa nafanya wizi huo.
Muongoza mashitaka, Mr Ahmed Ado, alimtupa jela muhusika mara baada ya kupatikana na hatia.
Ado, licha ya kumuhukumu kifungo cha miezi minne jela pia kwenye hukumu hiyo aliambatanisha na adhabu ya kufanya kazi ngumu na kuondoa uwezekano wa kulipa faini.
0 comments:
Post a Comment