Dec 26, 2013

Ikhwan Misri yawekwa katika orodha ya magaidi

Serikali ya mpito ya Misri inayoungwa mkono na jeshi imelitangaza kundi la Ikhwanul Muslimin kuwa ni la kigaidi na kupiga marufuku harakati zake zote.

Taarifa ya serikali ya mpito ya Misri imedai kuwa, uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa, kundi hilo ndilo lililotekeleza shambulizi la bomu katika eneo la Manousra siku ya Jumanne na kuwaua watu 16 na kujeruhi wengine 140. 


Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Hossam Eissa amesema, serikali na wananchi wa Misri wameshangazwa na jinai hizo za Ikhwanul Muslimin na kwamba kundi hilo halijali chochote isipokuwa machafuko.

Harakati ya Ikhawanul Muslimin imekanusha kuhusika katika shambulio la bomu la Manousra na kulaani kitendo hicho. 

Pia kundi la wanamgambo linalojiita Ansar Beit al Maqdis lilitangaza kuhusika katika shambulizi hilo lililotokea Jumanne ya wiki hii nchini Misri.

0 comments:

Post a Comment