Mkuu wa tume ya mabadiliko ya katiba
ya Misri amemkabidhi Rais Adly Mansour wa serikali ya mpito ya nchi
hiyo rasimu ya katiba mpya na hivyo kumpa fursa ya mwezi mmoja ya
kuitisha kura ya maoni.
Amr Moussa Katibu Mkuu wa zamani wa Arab League
amekabidhi rasimu hiyo ya katiba mpya hapo jana siku tatu baada ya
kamati ya watu 50 kukamilisha kazi yake ya kuiandaa.
Akizungumza na vyombo vya habari huko
Cairo, Amr Moussa amewataka Wamisri wote kushiriki kwenye kura ya maoni
na kuipigia kura ya 'ndiyo' rasimu hiyo.
Amesema Misri inakabiliwa na
vitendo hatari vya uchochezi ambavyo wanapasa kuvikomesha.
Amr Moussa
ametoa wito huo kwa wananchi wa Misri wa kushiriki kwenye kura ya maoni
na kupiga kura ya 'ndiyo' huku rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo
ikilizatiti na kulipa nguvu zaidi jeshi kimadaraka.
0 comments:
Post a Comment