DOCTOR SHEIKH IBRAHIM GHULLAM.
Idara ya madrasa DYCCC leo imeendesha usaili kwa waalimu wa madrasa wa mkoa wa Dar es alaam.
Usaili huo ulioanza saa tatu asubuhi na kumalizika saa saba na nusu umefanyika ndani ya msikiti wa Qiblatain uliopo Kariakoo Dar es salaam.
Akiongea na munira blog mara baada ya usaili huo mjumbe wa Idara ya Madrasa Sheikh Said Bawazir amesema,kimsingi usaili umekwenda vizuri na wana matumaini makubwa kwamba kupitia usaili huo tutawapata waalimu wa madrasa wenye uwezo na ubora.
Amesema,"kwa hakika nimevutiwa na hawa vijana kwani kuna mabadiliko makubwa,wengi wao ni vijana wa kidato cha sita,lakini wana elimu mzuri ya dini na wanaongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha mkubwa na wapo tayari kuutumikia uislamu kupitia nyanja hii ya ualimu wa madrasa"
Kwa upande wake Dokta Sheikh Ibrahim Ghullam ambaye alikua ni mmoja wa wasaili,amesema kimtazamo wa awali wengi wamefanya vizuri na wanaonekana wana hamu ya kusomesha lakini pia wana nia ya kujiendeleza.
Aliongeza kwa kusema kwamba wachache miongoni mwao wanakabiliwa na changamoto ya kushindwa kusema lugha ya kiarabu japo wana uwezo wa kusikia na kukielewa.
Dokta Ibrahim Ghullam aliitaka jamiii iwapokee na kuwapa nafasi waalimu watakaopita katika mchujo huo.
Kwa upande wake Sheikh Ramadhan kwangaya ambaye ni katibu mkuu wa idara ya madrasa amesema lengo la usaili huu ni kupata waalimu kumi watakao ingia katika udhamini wa Idara ya Madrasa DYCCC.
Matokeo ya usaili huo yanatarajiwa kutangazwa kabla ya Tarehe kumi mwezi huu.
Kwa sasa Idara ya Madrasa DYCCC imewadhamini waalimu 44.
SHEIKH KWANGAYA AMBAYE NI KATIBU MKUU AKIFUATILIA KWA MAKINI MCHAKATO WA USAILI.
MMOJA YA WASAILIWA AKIFANYIWA USAILI KWA NJIA YA SHAFAWI
USTAADH HAJJ JABU AKIJAZA MASWALI.
WASAILIWA WAKIWA MAKINI KUJAZA MASWALI.
MMOJA YA WASAILIWA AKIWAJIBIKA.
WASAILIWA WALITAKIWA KUZIWEKA KANDO SIMU ZAO.
0 comments:
Post a Comment