Mtuhumiwa
wa Mauwaji ya Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar Omar
Musa Makame amepewa dhamana katika mahakama kuu ya Zanzibar kutokana na
kutokamilika kwa ushahidi wa kesi hiyo.
Akitoa
dhamana hiyo Jaji Mkuu Omar Othman Makungu amesema mtuhumiwa huyo
amepewa masharti mawili; moja kuwa atalazimka kupata wadhamini wawili
watakoandika bondi ya laki tano kila mmoja wakiwa na vitambulisho vya
Mzanzibari Mkaazi (ZAN ID).
Na sharti la pili ni kuwa na barua ya sheha na kuripoti katika Mahakama mbele ya Mrajis Mkuu kila siku ya Jumatatu.
Mapema
mwendesha mashitaka wa serikali, Abdalla Issa Mgongo alidai mahkamani
hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo kesi hio
ipangiwe siku nyengine kwa kutajwa.
Nae
kwa upande wake Wakili anayesimamia kesi hiyo, Abdalla Juma aliomba
Mahkama hiyo kuwa muda umeshakuwa ni mwingi na ushahidi bado
haujakamilika hivyo ni vyema kesi hiyo kufutwa ikiwa haikuwezekana basi
mtuhumiwa apatiwe dhana.
“Kwa
kuwa muda umeshakuwa mwingi na ushahidi hadi hii leo haujapatikana basi
kesi ifutwe au Mtuhumiwa apewe dhama”alisema Wakili huyo Mahakamani
hapo.
Mwendesha
Mashitaka wa Serikali Issa Mgongo alipingana na ombi hilo la kutaka
kesi ifutwe na kusema ombi hilo hakubaliani lililotolewa na Wakili wa
upande wa Mtuhumiwa.
Alisema ombi la pili lifanyiwe kazi likizingatiwa mashati yatakayokubaliawa na mahakama.
Mtuhumiwa Omar
Musa Makame anadaiwa kumpiga risasi na kumuua Padre Mushi Februari 17
mwaka huu wakati akienda kuongoza Ibada ya Jumapili asubuhi katika
kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar . Alitiwa mbaroni Machi 17 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment