Dec 20, 2013

Wanawake wa Saudi Arabia wadai haki ya kuendesha magari kama wanaume

Mwanamke wa Saudi Arabia akiingia katika gari
Mwanamke wa Saudi Arabia akiingia katika gari

Nchi ya Saud Arabia huenda ikakumbwa na maandamano leo Jumamosi baada ya wanaharakati wanawake kutangaza kufanya kampeni endelevu ya uendeshaji magari, kupinga marufuku ya wanawake kuendesha magari katika nchi hiyo ya kifalme.

Awali wanaharakati hao walitangaza kuzindua kampeni ya kuendesha magari leo Jumamosi lakini wameahirisha baada ya vitisho vya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao,badala yake wametangaza kuifanya kampeni hiyo kuwa endelevu kuanzia leo.


Nchi ya Saudi Arabia ni nchi pekee duniani ambayo inapiga marufuku wanawake kuendesha magari na wanawake wanaokiuka marufuku hiyo hukamatwa na kufungwa.

Mwaka 2007 mfalme Abdullah alitangaz kuwa marufuku hiyo ni uamuzi wa kijamii uliofikiwa na raia wa nchi hiyo na hivyo serikali inatekeleza matakwa ya watu wake.

0 comments:

Post a Comment