Nov 30, 2013

Taasisi Ya Munira Kusherehekea MWAKA MPYA WA KIISLAM




Taasisi ya Munira Madrasa And Islamic Propagation Association kesho In Shaa Allah itafanya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa kiislamu 1435 HJR.

Akiongea na Munira blog Ustaadh Ally Jongo ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo amesema kwamba Sherehe hizo zitafanyika katika viwanja vya Munira Madrasa vilivyopo Magomeni Makuti kuanzia saa kumi jioni In Shaa Allah.
"Kupitia sherehe hizo tutawagawia ripoti wanafunzi wetu baada ya kufanya mitihani ya mwaka ambapo mbali ya kugawa ripoti lakini washindi wa mitihani tutawagawia zawadi maalum"Alisema.

Aliendelea kusema kwamba pia kutakuwa na michezo mbalimbali kwa rika tofauti na jinsia tofauti huku washindi wataibuka na zawadi nono.

"Lengo letu ni kuutangaza mwaka mpya wa Kiislamu kwa Waislamu wa maeneo haya ambao umekuwa si wenye kueleweka vizuri sana na ndiyo maana pia tutakuwa na maswali yanayo husu mwaka mpya na washindi tutawapa zawadi".

"Tunatoa wito kwa waislamu wa maeneo mbalimbali wajitokeze kwa wingi katika hafla hiyo"mwisho wa kumnukuu.

Katika sherehe hizo mgeni rasmi atakua Sheikh Ramadha Khamis Kwangaya ambae ni katibu wa Idara ya madrasa DYCCC.

Taasisi ya Munira Madrasa imekua na utamaduni wa kusherehekea mwaka mpya wa Kiislamu kila mwaka unaokwenda sambamba na kuwakabidhi ripoti wanafunzi baada ya kufanya mitihani ya mwaka.

0 comments:

Post a Comment