Nov 27, 2013

SHEIKH AISHI NA RISASI MWILINI KWA MWAKA MMOJA

huh 

Hali ya kiafya ya Sheikh Nimr al Nimr ambaye amewekwa kwenye seli ya mtu mmoja kwenye gereza moja nchini Saudi Arabia, inazidi kuzorota siku baada ya siku. 

Sheikh Tayseer Baqer, kaka wa Sheikh Nimr al Nimr ameeleza kuwa, serikali ya Saudi Arabia hadi sasa haijatoa ruhusa ya kuondolewa risasi iliomo ndani ya mwili mwa mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu baada ya kupigwa risasi na askari usalama wa nchi hiyo zaidi ya mwaka mmoja uliopita. 

Amesema kuwa, hali hiyo inatishia kukatwa mguu wa mwanachuoni huyo wa Kiislamu.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Sheikh Nimr alifyatuliwa risasi na kisha kutiwa mbaroni tarehe 7 Julai mwaka 2012 wakati alipokuwa akilalamikia vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoofanywa na utawala wa kifalme wa Saudi Arabia.

Mahakama ya Saudi Arabia ilimuhukumu Sheikh Nimr al Nimr adhabu ya kifo kwa tuhuma za kuchochea wananchi, kufanya njama za kuzusha ghasia, kuingilia mambo ya ndani ya Bahrain, kuukosoa utawala wa Saudi Arabia, kuharibu mali za umma na watu binafsi na kuitisha maandamano kinyume cha sheria.

0 comments:

Post a Comment