Nov 28, 2013

MALEZI MABAYA NI CHANZO CHA UHALIFU;IGP

IGP: Familia zidhibiti uhalifu


MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, amewataka wanafamilia nchini kujichunguza ili kubaini wahalifu na kuwashauri kuacha vitendo hivyo.

IGP Mwema alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhimiza na kuelimisha malezi bora kwa familia.

Alisema endapo familia haitatoa malezi bora kwa watoto wao, ndiyo chanzo cha kupata watoto wenye mmomonyoko wa maadili.

“Kuna tafiti mbalimbali ambazo zimebaini asilimia kubwa ya wazazi wengi hawatoi malezi yanayotakiwa kwa waototo wao ndiyo maana tumeona kuna umuhimu wa kuwaelimisha,” alisema.

Aliongezea kuwa kampeni hizo zina lengo la kuzuia vitendo vya kihalifu ngazi ya familia, kuwahimiza wazazi kuweza kutoa malezi bora kwa watoto ili waweze kuepuka vitendo visivyofaa. Pia aliwataka kina mama ambao ndio walimu wa familia kutoa elimu kwa jamii.


Mwema alisema kampeni hiyo itapunguza watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwamo uvutaji bangi, matumizi ya dawa za kulevya na biashara ya ukahaba, kwani yanaangamiza nguvu kazi za taifa ambao ni vijana.

0 comments:

Post a Comment