Nov 29, 2013

MAITI Azaa Mtoto Baada Ya Kunyongwa



Katika hali isiyo ya kawaida, watu wa mji wa Kaharisi nchini Uturuki wameshuhudia tukio la ajabu la kuzaliwa kitoto kichanga cha miezi saba baada ya mama yake kunyongwa. 

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa, mtoto huyo wa kiume amezaliwa akiwa na afya nzuri. 

Habari zaidi zinasema kuwa, daktari wa gereza aliukimbilia mwili wa Sabah Mosilibasa, mwenye umri wa miaka 28  baada ya kujifungua mtoto huyo, huku akikata roho. 

Aidha habari zinasema kuwa, hadi mwanamke huyo anatiwa kitanzi, hakuna aliyekuwa anajua kwamba alikuwa na ujauzito wa miezi saba, kutokana na unene wa mwili wake, suala ambalo limezidi kuwashangaza watu. 

Sabah alihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa sumu mumewe na watoto wake wawili na alisalia gerezani kwa muda wa miezi mitatu akisubiri hukumu dhidi yake. 

Duru za habari zinasema kuwa, watu walishangaa baada ya kuwekwa kamba ya kitanzi shingoni mwake na kufyatuliwa kitanzi, kama ishara ya kumalizika adhabu hiyo, lakini Mosilibasa aliendelea kutikisika miguu licha ya kwamba adhabu hiyo ilikuwa imemashatekelezwa dhidi yake. 

Muda mchache baadaye alizaa mtoto wa kiume ambaye awali alidhaniwa kuwa naye ameshakufa, lakini baada ya kumsaidia pumzi mtoto huyo aliweza kupumua na kisha kupiga ukelele.

0 comments:

Post a Comment