MZEE ABDUL AZIZ MUHAMED HASSAN (KUSHOTO) AMBAYE NI MMOJA WA WAGENI RASMI AKIWA NA MWENYEKITI WA BODI YA SHULE BWANA HASSAN AKRABI KATIKA MAHAFALI YA WAKHITIMU WA KIDATO CHA NNE YALIYOFANYIKA JANA SHULENI YEMEN CHANG'OMBE DAR ES SALAAM
Wazazi wametakiwa kuiepuka
migogoro baina yao
kwani inachangia kudumaza maendeleo ya kielimu kwa watoto.
Wito huo umetolewa jana
katika mahafali ya kuwaaga wakhitimu wa kidato cha nne wa shule ya DYCCC Sekondari iliyopo chang’ombe Dar es salaam.
Akiongea katika mahafali
hayo,Bwana Abdul Aziz Muhamed Hassan ambaye alikua ni mmoja wa wageni rasmi alisema watoto
wanategemea sana ushirikiano na msaada wa hali na mali kutoka kwa wazazi.
Akifafanua zaidi alisema msaada
huu wa wazazi hauishii katika kulipa ada tu,bali unaenea katika nyanja
mbalimbali ikiwemo kufuatilia maendeleo yao
sambamba na kukaa nao kwa lengo la kusikiliza shida zao.
Aidha aliwasihi wazazi
kuepuka migogoro na mitafaruku kati yao
isiyo ya lazima.
“Wazazi wenzangu,ni jambo lisilo epukika katika famila zetu wakati
mwengine kuwa na misuguano ya hapa na pale,tahadhari yangu kwenu ni kwamba tuiepuke
misuguano hiyo na ikibidi basi misuguano hiyo isiwahusishe watoto”alisema.
Aliendelea kusema kwamba “mitafaruku hii ikiwahusisha watoto itakuwa
na nafasi kubwa ya kuathiri maendeleo yao
ya kitaaluma na kimaadili”,mwisho wa kunukuu.
Jumla ya wanafunzi 74 wamekhitimu kidato cha nne shuleni hapo,kati hao 45 wakiwa ni wasichana.
Jumla ya wanafunzi 74 wamekhitimu kidato cha nne shuleni hapo,kati hao 45 wakiwa ni wasichana.
Shule ya DYCCC ilimpa heshima ya kuwa mgeni rasmi baada ya mtoto wake (Safia Abdul Aziz) kuwa ni mmoja ya wanafunzi wawili waliofanya vizuri.
MWENYEKITI WA BODI YA SHULE YA YEMEN HASSAN AKRAB AKIMKABIDHI CHETI MMOJA YA WAKHITIMU WA KIDATO CHA NNE.
MR ANTIPAS CHALE MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YEMEN AKIONGEA KATIKA MAHAFALI HAYO"KUNA DHANA KWAMBA SHULE ZA KIISLAMU ZINA TABIA YA KUFELISHA WANAFUNZI,DHANA HII SI SAHIHI NA TUKISHIRIKIANA TUNA UWEZO WA KUIONDOSHA KABISA"ALISEMA.

BAADHI YA WAKHITIMU WAVULANA WA KIDATO CHA NNE WAKIWA KATIKA MAHAFALI HAYO.
0 comments:
Post a Comment