Nov 29, 2013

Israel yawashambulia waumini Masjdul al-Aqswa

Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limewashambulia waumini katika msikiti wa al-Aqswa huko Baytul Maqaddas Palestina. 

Taarifa zaidi kutoka Baytul Muqaddas zinasema kuwa, jeshi la Israel likiwa pamoja na walowezi wa Kiyahudi limewashambulia waumini waliokuwa wakitekeleza ibada katika Msikiti wa al-Aqswa na kuwajeruhi makumi kati yao huku hali ya baadhi yao ikiripotiwa kuwa mbaya. 

Sheikh Azzam Khatib, Mkurugenzi wa Waqfu katika Masjdul Aqswa amesema kuwa, zaidi ya walowezi wa Kiyahudi 150 wakiwa pamoja na jeshi la Israel leo wamevamia msikiti huo kupitia mlango wa al-Maghariba na kuwashambulia waumini.

 Ameongeza kuwa, uvamizi huo ulipelekea kutokea mapigano baina ya pande mbili na kusababisha waumini wengi kujeruhiwa.

0 comments:

Post a Comment