Faida
ya kuomba Tawbah sio tu kughufuriwa madhambi yote Muislamu akajihisi
kuwa basi inamtosheleza kuwa hana dhambi tena, hapana si hiyo tu! Bali
pia kuna faida nyingi sana zaidi ya hiyo zinazomrudia mwenyewe mja anayeomba tawbah na ambazo bila shaka kila mtu angelipenda sana kuzipata faida hizo. Miongoni mwa faida hizo ni:
1-Kujaaliwa kupata starehe na fadhila kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى .
( وَأَنِ اسْتَغْفِرُواْ رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُواْ إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَى أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَه)
(Na
ili mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake.
Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu. Na Atampa kila
mwenye fadhila, fadhila Yake) [Huud: 3]
2-Kuletewa neema ya mvua na kuzidishiwa nguvu.
(وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُواْ رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُواْ إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاء عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَى قُوَّتِكُمْ وَلاَ تَتَوَلَّوْاْ مُجْرِمِينَ)
(Na
enyi watu wangu! Muombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie Kwake.
Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika, na
Atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu) [Huud:52]
3-Mbali ya mvua bali na kujaaliwa mali na watoto, na kupewa kila aina ya neema.
Nuuh (عليه السلام)
alipowalingania watu wake miaka kuwatoa katika shirki, aliwanasihi
waombe maghfirah na tawbah na akawatajia fadhila na faida zake:
(فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا) ((يُرْسِلِ السَّمَاء عَلَيْكُم مِّدْرَارًا) (وَيُمْدِدْكُمْ بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا)
(Nikasema:
Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe) (Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo) (Na Atakupeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakufanyieni mito) [Nuuh:10-12]
4- Kujaaliwa Pepo ya milele
(وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُواْ فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُواْ أَنْفُسَهُمْ ذَكَرُواْ اللّهَ فَاسْتَغْفَرُواْ لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ اللّهُ) (وَلَمْ يُصِرُّواْ عَلَى مَا فَعَلُواْ وَهُمْ يَعْلَمُونَ) (أُوْلَئِكَ جَزَآؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ)
(Na
ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka
Allaah na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao - na nani anayefuta dhambi
isipo kuwa Allaah? - na wala hawaendelei na waliyoyafanya na hali
wanajua) (Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao) [Aal-'Imraan:135-136]
Itaendelea wiki ijayo In shaa Allah……
0 comments:
Post a Comment