Nov 12, 2013

IKHTILAFU zetu Zisitugombanishe-SHEIKH KISHK

 SHEIKH NUURUDDIN KISHK AKIHUDHURISHA MADA KATIKA MSIKITI WA QIBLATAIN.

Waislamu nchini wametakiwa kutozipa nafasi Ikhtilafu zilizopo kati yao ili kulinda umoja wao.

Nasaha hizo zimetolewa na Sheikh Nuuruddin Kishki alipokuwa anahutubia katika Masjid Qiblatain mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alikiri kuwepo kwa tofauti za kielimu ambazo kwa bahati mbaya zimesababisha baadhi yetu kutengana.

Akitolea mfano Sheikh Kishki alisema,"baadhi yetu wanaipinga khitma kwa kuamini haimsaidii mar hum,lakini baadhi yetu wanaikubali khitma wakiamini inamsaidia mar hum,pande hizi mbili zote zipo sahihi kwa kuwa maimamu wetu wapo walioikubali na wapo walioikataa,sasa hili lisitugombanishe",alisema

Aliendelea kusema kwamba hakuna sababu ya kumuona mwenzako ni kafiri au ni mkosefu kwani hakuanza yeye,bali yeye kanukuu kutoka kwa maimamu na masheikh wetu wakubwa.

"Ndugu zangu jambo la msingi ni wewe kujikinaisha kwa hoja lakini pia uheshimu hoja ya mwenzako",alisema

Wakati huo huo Sheikh Kishki alionesha masikitiko yake kwa baadhi ya masheikh kuangalia mapungufu ya masheikh wenzao na kuyasema.

"leo imefikia hatua,baadhi ya masheikh wanasikiliza CD za masheikh wenzao kisha pale penye kosa ndipo wao wanaaza kushambulia,kwa kweli hili si jambo zuri na halijengi umoja wetu"Alisema kwa masikitiko.

Mihadhara ya kuukaribisha mwaka mpya wa kiislamu 1435 umeaandaliwa na kamati ya mihadhara ya Masjid Qiblatain chini ya usimamizi wa Sheikh Ally Bassaeleh.
 
 BAADHI YA WAUMINI WAKIMSIKILIZA SHEIKH KISHK
 

0 comments:

Post a Comment