Oct 5, 2013

World Islamic Call Society Yawafunda Waalimu Wa Madrasa.


MKURUGENZI WA WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY SHEIKH AHMAD MUHAMMAD AKIWAHUTUBIA WANA SEMINA KATIKA UZINDUZI WA SEMINA YA WAALIMU WA MADRASA ULIOFANYIKA LEO.
 
Taasisi ya World Islamic Call Society yenye makazi yake nchini Libya imezindua semina kwa waalimu wa Madrasa wa mkoa wa Dar es salaam.

Semina hiyo ya siku tatu imefunguliwa leo katika ukumbi wa Jaafar Comlex uliopo Upanga jijini Dar es salaam.

Akifungua semina hiyo Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo hapa chini sheikh Ahmad Muhamad amesema wameona waendeshe semina kwa waalimu wa madrasa kwa kuwa wao ndiyo watu bora.

Mtume S,A,W amesema “mbora wenu ni yule ambaye anajifunza Qur aan na kisha akawafundisha wengine,ndipo kwa kufahamu ubora wenu tukaona tuwapatie semina itakayo ongeza uwezo wenu wa ufundishaji”mwisho wa kumnukuu.

Aliendelea kusema kwamba licha ya Lugha ya kiaarabu kuenea zaidi na kutumiwa na watu zaidi ya milioni nne duniani,lakini ni lugha ambayo pia inatumika katika makanisa mbalimbali duniani kama lugha ya mawasiliano.

Mbali ya makanisa katika nchi za kiarabu kutumia lugha hii (ya kiaarabu),nchi ya Chadi,eretrea na hata umoja wa mataifa wanatumia lugha ya kiarabu na imeiwekea siku maalumu (Desemba 18 ya kila mwaka) kusheherehekea lugha ya kiarabu duniani.

Hivyo basi ni muhimu sana kwa waalimu wa madrasa na waislamu kwa ujumla kujifunza lugha ya kiarabu.

Awali akitoa tamko la makaribisho katika semina hiyo,sheikh twalib Ahmad alisema semina hiyo ina lengo maalum.

Aliyataja malengo hayo kuwa ni pamoja na kumfundisha mwalimu wa madrasa njia za ufundishaji,kuingia katika soma la kiarabu,malezi ya kiislamu na saikolojia ya watoto.

Masheikh mbalimbali wanatarajia kuhudhurisha mada katika semina hiyo wakiwemo sheikh Suleyman



 VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU WA WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY WAKIWA NA MASHEIKH KATIKA UZINDUZI WA SEMINA ULIOFANYIKA LEO HII.

 SHEIKH ALLY MBWERA AKITARJIM KHUTBA YA MGENI RASMI
 
 SHEIKH TWALIB AHMAD AKITOA TAMKO LA MAKARIBISHO
 
 USTAADH NUOURUDDIN KINGALU KUTOKA MADRASAT DAAR YA TEMEKE,AKISOMA QUR AAN KATIKA UZINDUZI WA SEMINA HIYO.
 BAADHI YA WAALIMU WASHIRIKI WA SEMINA HIYO WAKIFUATILIA KWA MAKINI YANAYOJIRI KATIKA SEMINA HIYO,


0 comments:

Post a Comment