Taarifa kutoka mjini Mombasa pwani ya Kenya zinasema
kuwa vijana wameteketeza kanisa katikaghasia ambzo zimezuka kufutia
kuuwa kwa muhuburi wa kiisilamu.
Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa kwenye
ghasia hizo.
Sheikh Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na washirika wake watatu.
Polisi wamesema kuwa muhubiri huyo alikuwa amehubiri katika msikiti uliohusishwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab.
Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku
wa kuamkia leo huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa
waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo.
Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika
msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia
aliuawa kwa kupigwa risasi.
Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa
wanarejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.
Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo.
Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa
Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.
0 comments:
Post a Comment