WATOTO watatu wakazi wa Kijiji cha Likombora, Kata ya Mihumo
wilayani Liwale, Mkoa wa Lindi wamefariki dunia papo hapo baada ya
kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa bomu.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Ephraem Mmbaga aliwataja watoto waliofariki kuwa ni Seleman Namwera (13), Latifu Bayi (12) na mmoja aliyefahamika kwa jina la Ponda (10).
Alisema kuwa Jumapili iliyopita mgambo wakiongozwa na mshauri wao, Meja Tiba walifanya mazoezi ya kulenga shabaha ya silaha huko kwenye Kijiji cha Kipule ambako mabomu matatu hayakulipuka na wakafanikiwa kuyaokota mawili na kuyateketeza.
Kwa mujibu wa Mmbaga, siku ya tukio wanafunzi hao wa Shule ya Msingi Likombora, walikwenda kucheza karibu na sehemu ya kulengea shabaha ndipo walipoliokota hilo bomu na kuwalipukia.
Alisema kuwa mmoja wao alichanwachanwa kiasi cha kutotambulika uso wake, na kwamba mabaki ya miili yao yalizikwa juzi.

0 comments:
Post a Comment