Za mwizi ni Arobaini,ndivyo inavyonekana baada ya watu wawili wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya utapeli , huku
mmoja akitumia kitambulisho kinachomtambulisha kuwa ni ofisa mwandamizi wa
Idara ya Usalama wa Taifa, wametiwa mbaroni jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo
ambalo liligusa hisia za watu wengine lilitokea juzi maeneo ya Kawe, wakiwa
katika Hoteli ya Picol Beach saa 2.30 Usiku baada ya kuwekewa mtego.
Watuhumiwa hao watanashati waliokamatwa katika tukio hilo wametambuliwa kuwa
ni Fadhili Hamisi Mafutari ambaye anadaiwa kutumia kitambulisho cha Idara ya
Usalama wa Taifa, kikiwa na jina la Kennedy Magige na picha yake.
Pia anatumia simu yenye namba 0654-084-445 iliyosajiliwa kwa jina
la Kennedy Magige, ingawa rafiki yake ambaye amekamatwa naye kwenye tukio hilo,
Tabula Abdallah Mayenga, alisema anamfahamu na jina lake, Fadhili Hamisi Mafutari.
Watu hao walikamatwa baada ya kuwekewa mtego na watu wanaodai
kutapeliwa na Mayenga katika tukio lililotokea Ijumaa, wiki iliyopita maeneo ya
Maua Resort Beach.
Akisimulia tukio hilo,
mmoja wa mashuhuda alisema baada ya kutapeliwa, walianza kuweka mtego na
kufanikiwa kumnasa Magige, kwa kutumia mtu mwingine aliyempigia simu na
kujifanya ana shida naye.
Mtoa habari wetu huyo, alidai kwamba wakati Magige anawafanyia
tukio hilo la
utapeli, hakuwa anafahamu kama wamebaki na namba yake simu na baada ya
kufuatilia, walibaini imesajiliwa kwa jina la Magige.
“Alipopigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwake pengine alidhani
amekutana na mjinga mwingine, hivyo walipanga wakutane Hoteli ya Picol Beach,”
alisema mtoa habari wetu.
Vyanzo vyetu hivyo, vilieleza kuwa Magige alifika hotelini hapo
akiwa na gari aina Land Cruiser Prado namba T445 BCY na kisha kukutana
na mtu aliyekuwa amepanga naye, bila kujua alikuwa anaingia mtegoni.
Baada ya kufika, alitiwa mbaroni pamoja na mwenzake na kuanza kushushiwa
kipigo kikali na wananchi wenye hasira, ambapo ilibainika anamiliki
kitambulisho kinachomtambulisha kuwa ni ofisa mwandamizi Idara ya Usalama wa
Taifa.
Lakini alipohojiwa, Magige alijitambulisha kuwa yeye ni
mfanyabiashara wa mazao aina ya nafaka kauli ambayo ilitofautiana na rafiki
yake ambaye alikamatwa naye kwenye tukio hilo,
kwani alisema Mafutari (Magige) ni mfanyabiashara wa magari.
Mayenga alisema yeye ni fundi seremala na
kwamba alifika hotelini hapo kufuata hela kidogo kwa rafiki yake,lakini ghafla
aliona watu wanaanza kumfuatilia na hakuwa na njia ya kukimbia kwani alihisi
ataitiwa mwizi.
Baada ya watu hao kupata kipigo kutoka kwa
wananchi, walifika Polisi ambao waliweza kubaini kitambulisho hicho cha usalama
wa taifa, lakini Magige alipohojiwa alikana kuwa si mali yake.
Watuhumiwa hao waliondolewa eneo la tukio kwa
kutumia gari la Polisi namba T 332 ANV aina ya Land Rover Difender.
Akisimulia
tukio la kutapeliwa na mtu huyo, anayedaiwa kuwa usalama, shuhuda mmoja alisema
akiwa na dada yake Ijumaa iliyopita maeneo ya Maua
Resort Beach,
Kunduchi alifika mtu huyo, ambapo alijifanya kama
anawafahamu hivyo wakawa wamekaa wote.
Mtu huyo, alianza kuwauliza habari za siku
nyingi yeye na dada yake, wakati huo wakinywa soda. Alisema mtu huyo, inasemekana
aliwawekea kitu kinachodhaniwa ni dawa za kulevya kwenye kinywaji chao, kwani
hali zao zilibadilika.
Alisema dada yake huwa anasumbuliwa na
ugonjwa wa moyo, hivyo ghafla alianza kuhisi miguu kumwishia nguvu, ndipo
alipowaambia aende kwenye gari yake ili apate kiyoyozi na walifanya hivyo.
Shuhuda huyo alisema Magige alianza kuwauliza
kama wana kadi za ATM, kwani yeye hana, lakini
kuna mtu anataka kumtumia fedha kutoka Arusha.
Walipomwambia itawezekanaje muda
huo usiku, aliambiwa kuwa Arusha wanachelewa, ndipo walikataa na hapo kuanza
kumtilia shaka.
Baada ya hapo, shuhuda huyo anaeleza kwamba
alianza kumpora dada yake vitu alivyokuwa navyo na kurudisha gari nyuma kwa
kasi na kuanza kuondoka na ndugu yake huyo.
Alisema na yeye alikuwa na gari,
hivyo alianza kumfukuzia lakini alipofika maeneo ya Mtongani, aliishiwa nguvu,
hivyo ilibidi aende kutoa taarifa Polisi Mtongani.
Alisema mtuhumiwa huyo,alienda na dada yake
hadi maeneo ya hoteli moja (jina tunalo), ambapo alitaka kumtelekeza, lakini
alipiga kelele kuomba msaada ambapo walianza kulifukuza gari hilo kwa Bajaj, lakini alifanikiwa kuwaacha,
hivyo ndipo alipokumbuka namba na kuwapigia na kukutana nao Polisi, Mtongani.
ANAYEDAIWA KUTAPELI AKILA KICHAPO
0 comments:
Post a Comment