SHEIKH KILEMILE AKIJIBU SWALI LA MWNA SEMINA.
Waalimu wa Madrasa wanao shiriki Semina ya umuhimu wa kujifunza na kutumia Lugha ya Kiaarbu wametakiwa kuazimia kubadilika.
Hayo yamesmwa leo hii na Sheikh Suleiman Amran Kilemile alipokuwa akitoa jibu la ziada kwa swali lilioulizwa katika semina hiyo.
Alisema waalimu wa madrasa kutumia muda na siku nyingi katika wiki kwa ajili ya burdani ya kupiga dufu,huu ni muanguko wa kifikra.
"Ndugu wana semina,kutumia muda mwingi kuwafundisha watoto mambo ya burdani na kupiga dufu ni muanguko wa kifikra na kiakili".alisema.
"Sikatai,nafsi yoyote inahitaji burdani (iliyo halali),sisi wakati tuna soma,ilikuwa kila Al khamisi tunapiga dufu,na lengo lilikuwa ni kuwavuta watoto waje kusoma"Alisema
Sheikh Kilemile aliongeza kusema kwamba"lakini sasa dufu na burdani imekuwa kila siku,nawaomba tubakie na siku moja ya burdani,basi tutumie semina hii kuazimia kubadika",kauli ambayo iliungwa mkono na Sheikh Twalibu.
0 comments:
Post a Comment