Tarehe 31/08/2013 wanaskaut wa shule ya Qiblatain English
Midium Primary School waliwatembelea yatima wanao lelewa katika kituo cha hisani
kilichopo mbagala maji matitu,manispaa ya Temeke Dar es salaam.
Viongozi wa Qiblatain Skaut na wanaskauti wenyewe kwa pamoja
walishiriki kuwafariji yatima hao kwa kuwapa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula,nguo,vinywaji,vitabu,madawa na Pesa taslimu Shilingi laki mbili na
elfu sita.
Kwa mujibu wa kiongozi wa wana skaut wa Qiblatain mwalimu Omar Mavula amesema
ni “utamaduni wa shule hii kufanya mambo
ya kijamii mara kwa mara,mbali ya malengo mengine ya kuwafariji walengwa lakini
pia tunafanya haya kwa lengo la kuwajenga watoto wetu wawe na moyo wa uzalendo
na huruma kwa jamii yenye shida mbalimbali,na kwa hili tumefanikiwa kwani hivi
vitu vyote unavyoviona hapa wamenunua wanafunzi wenyewe”alisema.
PICHA ZIFUATAZO
ZINATOA TASWIRA HALISI YA TUKIO ZIMA LILIVYOKUWA.
HIVI NI VITU MBALIMBALI VILIVYOKUSANYWA NA WAN SKAUT WA QIBLATAIN VIKIWA TAYARI KWA SAFARI YA KUELEKEA MBAGALA MAJI MATITU KWA AJILI YA KUWAFARIJI MAYATIMA.
HAPA WANASKAUT WA QIBLATAIN WAKIINGIZA MIZIGO TAYARI KWA SAFARI.
"WEWE NI NDUGU YANGU,NIPO PAMOJA NA WEWE,USIHUZUNIKE EEE"NDIVYO ANAVYOONEKANA KUSEMA MWANAFUNZI ASIA RAMADHAN KWANGAYA KUTOKA QIBLATAIN SCHOOL.
HUYU NI MMOJA WA WALIMU WA QIBLATEN AKIWA AMEMBEBA MMOJA WA YATIMA WAKATI WALIPO WATEMBELEA KWA DHAMIRA YA KUWAFARIJI