- ASEMA NI UNYAMA MKUBWA MNO ULIOPO ZANZIBAR
- WANADHALILISHWA NA KUNYANYASWA.
- WANAONANA NA FAMILIA ZAO KWA TAABU.
- AVITUPIA LAWAMA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KWA UPOTOSHAJI.
Na waandishi wa munirablog;
Waislamu wa Tanzania wametakiwa kuunganisha nguvu ya pamoja
kuwakomboa Masheikh na Waislamu wengine takriban wapatao khamsini walioko
magerezani visiwani Zanzibar na hapa Tanzania
bara.
Wito huo umetolewa jana na
katibu wa kamati ya kutetea Haki za waislamu Tanzania sheikh ponda issa ponda
alipokuwa anawahutubia waislamu waliofurika katika msikiti wa kichangani ikiwa
ni katika sherehe za baraza la idd.
"Amesema nimekwenda Zanzibar,nimekaa
kwa siku tatu nikapita katika magereza ambayo Masheikh wetu
wamezuiwa,nikakutana nao,nikaongea nao,kwa hakika kwa mujibu wa maelezo yao na
kwa namna nilivyowaona,ni dhahiri ya kwamba wanafanyiwa unyama wa hali ya juu, wanadhalilishwa,wananyimwa haki za
msingi,sasa hawa ni ndugu zetu tena sote tupo katika taifa moja,ni lazima
tuunge nguvu zetu kuhakikisha tunawakomboa,kwani kilichopo hivi sasa ni dhulma ya
wazi ambayo hatupaswi kuivumilia".mwisho wa kumnukuu.
Hakuna sababu ya msingi
inayopelekea masheikh wetu hadi leo hii wawe magerezani,kwani wameuwa?hata hao
waliokamatwa kwa tuhuma za mauwaji sasa wako njee,ndugu zangu hakuna njia ya
itakayo tusaidia ila ni kuunganisha nguvu zetu sisi waislamu wa bara na
waislamu wa Zanzibar kuhakikisha tunawakomboa ndugu zetu hawa.
“Hili tatizo haliishii kwa masheikh na
maimau wetu tu,bali hata maamuma nao wankoseshwa haki za msingi za kuwasikiliza
masheikh wao ambao wapo magrezani,ndugu zangu hebu fikirini,sheikh farid,sheikh
mselem na wengineo,hawa wana darsa zao wanawafundisha waumini wao lakini katika
mwezi mzima wa ramadhan darsa hizi hazikuendeshwa kwa kuwa masheikh wao wapo
ndani,sasa hii ni dhulma isiyovumilika”alisema
Kwa upande mwengine Sheikh
ponda alivilaumu baadhi ya vyombo vya habari kwa kupotosha ukweli,"mimi
nilikwenda Zanzibar na nimekaa kwa siku tatu,nilikuwa natembea barabarani tena
kwa miguu,nimeswali katika misikiti mbalimbali,nimekwenda kuwaona masheikh wetu
waliopo magerezani,halafu baadhi ya vyombo vya habari eti vinasema nimejificha
na vyengine vinasema nimekimbia,huu ni upotoshaji." aling'aka Sheikh Ponda.
Tunawaomba ndugu zetu wa habari,waripoti
matukio kwa uhalisia na si vinginevyo.
Kumekuwa na wimbi la
kuwakamata na kuwasweka ndani masheikh na waislamu kwa madai mbalimbali na hata
kuwanyima dhamana au kuweka masharti magumu ya dhamana kitu ambacho waislamu
wanahisi ni uonevu dhidi yao.
HAWA NI BAADHI YA WAUMINI WALIOFURIKA KATIKA MSIKITI WA KICHANGANI JANA KUFUATILIA BARAZA LA IDD