Aug 9, 2013

Swala ya Idd el fitri yafana

  • MISIKITI YAFURIKA,VIWANJA NAVYO VYA FURIKA.
  • WAISLAMU WASISITIZWA UMOJA

Na waandishi wetu wa munirablog.
Waislamu nchini wameungana na Waislamu wengine duniani kwa kuswali swala ya iddil fitri baada ya kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan hapo jana.

Kwa mujibu wa waandishi wetu kutoka maeneo mbalimbali wameeleza kwamba Waislamu walijitokeza kwa wingi katika misikiti mbalimbali na maeneo ya wazi kwa ajili ya kuswali swala ya Idd.

katika viwanja vya Barafu vilivyopo katika shule ya msingi magomeni,iliswaliwa Swala ya Idd iliyohusisha misikiti minne ya maeneo hayo ambayo ni Masjid Tawwab,Masjid Haqiir,Masjid Ndugumbi na Msikiti wa Kiyonga uliopo Moroko Hotel ambapo kutokana na waumini kufurika uwanja ulionekana kuwa mdogo.


Katika khutba ya Swala ya Idd iliyosomwa na Sheikh Mbaramwezi aliwasisitiza waislamu kuwa na umoja.

Aidha jioni hii katika uwanja huo kuna michezo mbalimba inaendelea ambapo kesho kutakuwa na mechi ya mpira wa miguu baina ya masheikh na maustaadh wa misikiti na madrasa za magomeni makuti dhidi ya masheikh na maustaadhi wa misikiti na madrasa za magomeni ndugumbi.

Aidha wakati huu tunaporusha hewani habari hizi baraza la idd linaendelea katika msikiti wa kichangi magomeni mapipa ambapo kwa mujibu wa waandishi wetu waliopo ndani ya msikiti huo wanasema kwamba Profesa Lipumba ndiye anawasilisha mada huku jopo la mashekh lipo na mada mzito zinatolewa.

Tutawajulisha mara tu baraza la Idd litakapomalizika Inshaa Allah   




 BAADHI YA WAUMINI WALIOSHIRIKI IBADA YA SWALA YA IDD ILIYOFANYIKA LEO KATIKA UWANJA WA BARAFU ULIOPO SHULE YA MSINGI MAGOMENI JIJINI DAR ES SALAAM