Aug 31, 2013

MANSUOR HIMID KUPASUA JIPU!


Hivi ndio alivyopokelewa Mansour Yusuf Himid katika Mkutano wa Kamati ya Maridhiano hapo Bwawani.

Umati mkubwa wa Wazanzibar wamefurika katika ukumbi wa Bwawan Hall kufuatilia mjadala utakaoendeshwa na Kamati ya Maridhano juu ya mustakbali wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa mpashaji wetu ni kwamba muda huu Bwawan Hall limeshasheheni wengi wakiwa na shauku kutaka kujuwa hasa kufuatia kufukuzwa uanachama katika chama chake mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo. Huyo ni Bw Mansour Yussuf Himid ambaye hivi karibuni Chama cha Mapinduzi kulimfukuza uanachama. Uamuzi ambao wengi waliona haukustahiki kwa vile ni haki yake kisheria kutoa maoni juu ya katiba mpya kama vile mwenyewe anavyoona. 
 MANSUOR YUSUPH HIMID,KADA ALIYEVULIWA UANACHA WA CCM.

Aidha wakati huo huo Mwanaharakati Maarufu Bw Mohamed Riami (Eddy Riami) ametangaza kujiondoa katika Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza katika Kongamano lililotayarishwa na Kamati ya Maridhiano, hii ilikuwa strong speech iliyowahi kutolewa na Bw Eddy Riami amesema yeye sio mwanasiasa, akiwafananisha na Jusa na Mzee Moyo. Bali yeye ni raia kama walivyo raia wengine. 
Amewataka Wazanzibar kujitolea kutafuta heshma zao na nchi yao. Alisema kwamba ni wao ndio waliompigia kura Rais kwani Rais mwenyewe hakupiga kura katika uchaguzi uliopita. Hivyo anajuwa vipi Zanzibar itashinda kabla ya mwaka 2015. Alikuwa akikariri moja ya hotuba ya Mzee Karume alpokuwa anakadiria kuwa Zanzibar haihitaji uchaguzi
hadi baada ya miaka 50.

Ametaka suala la siasa litolewa katika katiba mpya. Vilevile amewataka viongozi wengine kuachana na siasa badala yake kupigania Zanzibar nje ya siasa. Kwani ni siasa ndio iliyoifikisha hapa Zanzibar.