MATAIFA 70 WASWALI IDD LEO,
- AFRIKA KUSWALI KESHO PAMOJA OMAN.
- NCHI YA NAIJA,INDIA NA INDONESIA ZA SWALI JANA.
Na mwandishi wetu wa
munira.
Imeelezwa kwamba leo nchi
sabini zimeswali swala ya iddil fitri baada ya kumaliza ibada ya funga ya
Ramadhan.
Hayo yameelezwa na Katibu
mkuu wa jopo la Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania Sheikh Khamis Mataka
alipokuwa anazungumza katika kipindi cha Ramadhan kareem kinachoendeshwa na Sheikh
Muhammad Idd kupitia luninga ya Channel Ten.
“Ingawa imepishana na mahesabu ya
falaq lakini nchi ya NAIJA,INDIA
katika mji wa kirara na INDONESIA
leo (Kwa maana jana tarehe 07/08/2013) wameswali Swala ya Idd”,alisema.
“Kwa nchi ya Saudi
Arabia wao wataswali kesho (kwa maana leo) japo mamlaka
ya Saud Arabia iliwatangazia waumini wake jana
(kwa maana juzi tarehe 06/08/2013) waangalie mwezi ingawa wao hiyo juzi ilikuwa
ni mwezi ishirini na nane”,mwisho
wa kumnukuu.
Aliendelea kusema kwamba
katika mataifa 70 yatakayo swali kesho (kwa maana leo) yamegawaniyika katika makundi
matatu,kundi la kwanza ni kundi lenye mataifa 17 ambao walianza kufunga jumanne
ya tarehe 9,kundi la pili la nchi 41 ni la wanaoifuata Saudia Arabia na kundi
la tatu ni nchi ya Uturuki ambao wao wanafunga kwa mahesabu na sio kuuona mwezi.
Nimeshangazwa kuona kwamba
ikiwa ni kweli madai ya unapoonekana mwezi katika nchi moja basi wanalazimika
watu wa mataifa mengine kufunga,mbona leo (jana) nchi ya JAINA na baadhi ya
miji katika inchi ya INDIA na INDONESIA wameswali Iddi kwa madai wameuona mwezi
na Saudi Arabia hawakuswali,lakini kinachonishangaza zaidi iweje jana (juzi)
mamlaka ya Saudii Arabia iliwatangazia waumini wake wautazame mwezi ilhali ni
mwezi ishirini na nane,alihoji Sheikh mataka huku akiiweka wazi web site yenye
kubainisha hayo kuwa ni “www,moonsiting.com”
Kwa upande wake msomi
mashuhuri nchi ambaye pia ni mhadhiri wa chuo kikuu morogoro Sheikh Muhammad Abdul
rahman Dedesi akichangia katika kipindi hicho alisema,”si muhimu mimi na wewe kujuwa
lini mwezi umeandama,kwa mujibu wa sheria za kifiqihi jukumu hilo ni la kamati
au mabaraza ya mwezi,shekh Muhammad nikwambie jambo la msingi,mwezi hautangazwi
na radio au kituo cha televishen,mwezi unatangazwa na mamlaka ya kufuatilia
mwezi katika taifa husika na waumini wa taifa hilo wanapaswa kufuata na
kutekeleza maelekezo ya mamlaka ya kufuatilia na kuutangaza mwezi katika taifa
husika,hebu nikupe mfano,leo wewe unaswali katika msikti wa Qiblaten pale
kariakoo,upo ndani ya swala unamsikia Suddays anaswalisha katika msikiti wa
mtoro anasema ALLAHU AKBAR anarukui,utamfuata huyo Suddays au utamfuata imamu
anaye kuswalisha hapo Qiblaten”mwisho wa kumnukuu.
Katika hali ya kukinaisha
maelezo,alitoa mfano mwengine ,”ikiwa umemuoa mwananmke,basi atalazimika
kusikiliza na kufuata maelekezo yako na wala halazimiki kusikiliza wala kufuata
maelekezo ya mume wa jirani yako”alisema.
Alikhitimsha kwa kusema
kwamba “Baraza la kifiqihi la kiislamu ulimwenguni lilikaa na kutoka na maamuzi
ambayo naomba niwasomee,kwamba suala la kuuthibitisha mwezi muandamo liachwe
kwa mamlaka ya ofisi ya kadhi au mufti wa kila nchi husika”.mwisho wa
kumnukuu sheikh dedesi.
Awali akizungumza kwa niaba
ya Mufti wa Tanzania,Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum alisema
wamewasiliana na watendaji wao kutoka katika vitongoji mbalimbali na
kuwasiliana na makadhi na mufti wa nchi za Afrika mashariki na kujiridhisha
kwamba mwezi haujaandama na hivyo waislamu wanawajibika kufunga kwa kukamilisha
idadi ya siku thelathin.
SHEIKH KHAMIS MATAKA KATIBU MKUU WA JOPO LA MASHEIKH NA WANAZUONI WA KIISLAMU WA TANZANIA,AKIONGEA KATIKA KIPINDI CHA 39 CHA RAMADHAN KAREEM KILICHORUSHWA LIVE JANA KUPITIA LUNINGA YA CHANNEL TEN