Jun 15, 2013

Wanafunzi wa Madrasa za Mkoa wa Dar Es salaam wafanya Mtihani wa Pamoja.

  • WAAHIDI KUFANYA VIZURI.

Hatimaye ile siku ikiyosubiriwa kwa hamu na wanafunzi wa madrasa mbalimbali zilizo chini ya udhamini wa taasisi ya kijamii ya DYCCC,imefika ambapo leo hii wameanza kufanya mitihani yao ya mwaka.

Mitihani hiyo ya siku moja inafanyika katika shule ya DYCCC iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam.

Mwandishi wa munira blog alifika maeneo hayo na kukuta viongozi waandamizi wa DYCCC na wasimamizi wa mitihani hiyo wakiwa katika heka heka za kuwahakiki watahiniwa na kuwapanga katika vyumba vyao vya mitihani zoezi ambalo lilichukuwa muda mrefu na kulazimika mitihani hiyo kuanza saa 3;48 badala ya saa 2;30 kama ratiba ilivyoenyesha hapo awali.

Tatizo hili limetokana na baadhi ya madrasa kuchelewa kuwaleta wanafunzi wao,lakini pia hatujawa na uzoefu bado sisi ni wachanga katika hiliuna,alisema sheikh Ramadhan Kwangaya ambae ni katibu mkuu wa idara ya madrasa ambao ndiyo waandaaji wa mitihani hiyo.

Kwa upande wake uUtaadh Zahirina Mussa Muswarrif kutoka kinondoni alisema tatizo la kuchelewa kuwafikisha watoto katika kituo kimetokana na baadhi ya wazazi kutotilia maanani jambo hili,"utakuta mtoto siku ya kwenda shule anaamshwa na saa moja yupo kituo cha basi,leo hii nimelazimika nikawaamshe baadhi ya wanafunzi makwao baada ya kuona wanchelewa kuja chuoni,sasa hii inanyong'onyesha,inabidi wazazi na walezi watuunge mkono katika hili kwani ni jambo ambalo linanyanyua kiwango cha elimu,mwisho wa kunukuu kauli ambayo iliungwa mkono na Ustaadh Sharifu wa Madrasat Afswahiyyah iliyopo Magomeni mtaa wa dosi.

Katika hatua nyengine wanafunzi waliofika kwa ajili ya mitihani hiyo walionekana wana kiu ya mitihani kulikoambatana na kujiamini kwa kiasi kikubwa,

"Muhula uliopita nilishika nafasi ya tatu,nimesoma vizuri,nimejiandaa vizuri na leo asubuhi nimesoma dua,nina hakika nitafanya vizuri kuliko nilivyofanya katika muhula uliopita",haya yalikuwa ni maneno ya Mwahija Bint Muharram Urembo mwenye umri wa miaka 14,mwanafunzi wa Madrasat Taalim ya Ilala Kota inayoongozwa na Sheikh Muhammad Kattan.

Rashid Ally Seyf ni mwanafunzi wa Madrasat Ammar Bin Yasir ya mbagara jijini Dar es salaam ambaye yupo Swafful khaamis (Darasa la tano) alisema ana changamoto kubwa zinazo mkabili ikiwemo ugumu wa masomo ya Taj-wiid,Tawhiid na Qiraa,lakini pamoja na hivyo atahakikisha anavunja rekodi ya mwaka jana ambapo alishika nafasi ya nne katika mkoa wa Dar es salaam kwa wanafunzi wa darasa la nne mwaka jana.
.
Munirablogspot ilikutana uso kwa uso na Sitti Haidar Twahir mwanafunzi wa Madrasat Afswahiyyah ya Magomeni Mapipa mtaa wa Idrisa,aliyeonekana kuwa na uwezo mzuri wa kujieleza,yeye alisema,nimesikia kwamba mwaka jana nimefanya vizuri,lakini sijaambiwa wala kuona nimekuwa mtu wa ngapi,japo nina kiu ya kuona matokeo yangu ya mitihani,lakini hii haiwi kikwazo cha kufanya vizuri katika mtihani huu,kwani najiamini nimeyaelewa vizuri masomo yetu na kwa uwezo wa mungu nitaiwakilisha vyema madrasa yangu na kulinda heshima yangu binafsi,alisema binti huyo.

Kauli yake ya kutokupewa au kutajiwa matokeo ya mitihani,ilimfanya mwandishi wetu amtafute ustadh wake (Ustaadh sharif) ambae alikiri uongozi kutokuwapatia au kuwatajia wanafunzi wake matokeo ya mtihani uliopita na kusema hili linaweza kuzungumzwa zaidi na mudiir aliyemtaja kwa jina moja la ustadh Bakari.

Mwanafunzi Mulhat Bint Abdallah Bin Abdul rahman mwenye miaka 11 anayesoma darasa la nne katika Madrasat Mus ab Bin Umayr ya Uzuri Sinza,aliwaomba idara ya madrasa DYCCC wawapatie kitabu cha Ta'aliiq kwani amedai wamesomeshwa bila ya kupewa vitabu hivyo na kuhisi kwamba somo hilo linaweza kumpunguzia kasi na nia yake ya kuvunja rekodi aliyoishika mwaka jana kwa kushika nafasi ya nne kwa wanafunzi wa ,aidha alionesha kutofurahia tabia ya baadhi ya wanafunzi kwa kuchungulia majibu ya wenzao na kuwataka wasimamizi wawe makini na hali hiyo.

Aidha munirablog spot,libahatika kuhojiana na baadhi ya wasimamizi wa mitihani hiyo akiwemo Sabbaha Makusi ambaye licha kufurahishwa na utaratibu huo wa mitaani lakini alishauri changamoto zipunguzwe kwa haraka kwani si rahisi kuziondosha zote.

Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na uduni wa posho za waandaaji na wasimamizi wa mitihani,kwani usalama wa mitihani upo kwa watu hawa,sasa ni vyema waangaliwe vizuri,alisema

Mwandishi wa blog ya munira akiongea na waalim kadhaa waliowaleta wanafunzi wao kwa ajili ya kufanya mitihani hiyo walisema,iwapo idara ya madrasa dyccc itabadili mfumo wa udhamini kutoka uliopo hivi sasa wa kumdhamini mwalimu mmoja wakati madrasa ina walimu zaidi ya mmoja,na badala yake ikawadhamini walimu wa madrasa yote,tunaimani kiwango cha elimu kitaboreka zaidi ya hapa,,"unajuwa ndugu mwandishi leo posho tunayoipata ya kila mwezi ina sababisha fitna kubwa sana kwetu,ninacho kipata mimi nawagawia wenzangu japo kidogo,kwa sababu ushirikiano wao katika madrasa yetu ni mkubwa,lakini baadhi yao wanahisi mimi napata kikubwa zaidi na mwishowe sehemu kubwa ya majukumu wananiachia mimi,kwa kweli huu ni mtihani,alisema ustaadh Abbas Salum wa Madrasat Qaadiriyyah iliyopo Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa idara ya madrasa DYCCC alipoulizwa na mwandishi wa blog ya munira juu ya madai hayo ya udhamini,alikiri kulifahamu,"ni kweli hilo tumeliona na hatuna shaka nalo,tumenza kujipanga kwa lengo la kulitafutia ufumbuzi".mwisho wa kunukuu

Hadi mwandishi wa munira blog anaondoka eneo la tukio wanafunzi tayari wameshaanza mitihani hiyo.


Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika uhakiki muda mfupi kabla ya kuingia madarasani kuanza mitihani leo hii.
Hawa ni sehemu ya wanafunzi wa madrasa za mkoa wa Dar es salaam wakifanya mtihani.

Msimamizi wa mitihani akionekana kufuatilia kwa makini utendaji wa watahiniwa.

Baadhi ya wanafunzi wa madrasa wakionekana kushughulishwa na mitihani.

Picha na habari kwa mujibu wa mwandishi wa munira.

0 comments:

Post a Comment