Jun 14, 2013

Wanafunzi Wa Madrasa kufanya Mitihani ya Pamoja Kesho.


  • IMEANDALIWA NA IDARA YA MADRASA D Y C C C.
  • MORARI WA WANAFUNZI UPO JUU.

Habari na mwandishi wa munira
Wanafunzi wa madrasa za mkoa wa Dar es salaam zinazo dhaminiwa na Idara ya Madrasa D Y C C C ,Inshaa Allah kesho wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya mwaka.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa idara  hiyo Shekh Ramadha Khamis Kwangaya amesema maandalizi yote yamekamilika kilicho baki ni siku na saa ya kuanza mitihani.

kwa upande wake ustaadh Ramadhan A.Ramadhan wa Madrasat Tarbiyah Islamiyyah ya mtaa wa Idrisa Magomeni Mapipa jijini Dar es slaam amesema,wanafunzi wake wapo vizuri wanasubiri wakati ufike na wafanye kitu walichowafundishwa kisha watasubiri hukumu.

"Unajuwa sisi ni kama makocha,tumewaandaa vijana vizuri sana na hata katika mitihani yetu ya ndani wamefanya vizuri na wameonyesha ushindani mkubwa ambao unanipa matumaini ya kwamba historia itajiuridia"mwisho wa kumnukuu.

Madarasat Tarbiyya ndiyo iliyoibuka washindi wa jumla katika mitihani ya mwaka jana.

Akiendelea kuongea kwa njia ya simu na mwandishi wa blog ya munira leo hii hivi karibuni ,Ustaadh Ramadhan alisema kuna kila sababu ya kuipongeza idara ya madrasa D Y C C C  kwa utaratibu huu wa kihistoria kwani ni utaratibu unaokuza elimu na kuleta ushindani kwa wanfunzi.

Aidha alishauri dosari ndogondogo zipatiwe ufumbuzi mapema ili kuepusha kutokushusha morari wa wanafunzi na walimu ambao kwa sasa upo juu mno.

Alisema "unahitajika umakini wa hali ya juu katika usahihishaji wa mitihani na kuitunza hiyo mitihani ili mwisho wa siku kila mtahiniwa apewe mitihani yake ikiwa imetimia".

Alipouliwa na mwandishi wa blog ya munira kwamba zawadi zilizotolewa mwaka jana zimekidhi haja,ustaadhi Ramadhan alijibu,"Nimewaandaa wanafunzi wangu kufuzu katika mitihani hiyo,sijawaanda kuchukuwa zawadi,kwani lengo la mitihani ni kupima uwezo wa wanafunzi,lakini alisema zawadi zinazotolewa kwa madrasa iliyoshinda ni vyema ilingane na idadi ya walimu wanaosomesha katika madrasa husika kwani umoja na ushirikiano wa walimu hao ndiyo unaopelekea madrasa husika kufanya vizuri na siyo juhudi pekee za mwalimu aliyedhaminiwa"mwisho wa kumnukuu.

Kwa wiki mzima mwandishi wa blog ya munira aliwashuhudia watendaji wa idara ya madrasa D Y C C C wakihaha kuhakikisha  maandalizi na yanayoambatana na mitihani hiyo yanakwenda vizuri hali iliyowalazimu baadhi yao watendaji hao kulala ofisini ili kukamilisha lengo.


"Alhamdu lillaah tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kufanikisha tuliyoyakusudia",alisikika Ustaadh Daud Abuobakr ambaye ni katibu muhtasi wa idara hiyo,alipotembelewa na mwandishi wetu na kukutwa akiwa katika hatua za mwisho za maandalizi hayo hivi punde.

Mitihani hiyo itafanyika kesho kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa Al asri katika shule ya D Y C C C iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam na inatarajiwa kuwashirikisha wanafunzi 850 kutoka madrasa mbalimbali za mkoa huu.
Pichani juu ni Sheikh Ramadhan Khamis Kwangaya ambaye ni katibu mkuu wa idara ya madrasa DYCCC.

0 comments:

Post a Comment