WAISLAMU WATAKIWA KUUHESHIMU MWEZI WA RAMADHAN
- SISI TUSIPOUHESHIMUSISI WASIO WAISLAMU HAWATOUHESHIMU,
- TUJIEPUSHE NA KUVUNJA JUNGU.
Waislamu wametakiwa wauheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Hayo yamesemwa usiku wa kuamkia leo na Mhadhiri maarufu hapa nchini Sheikh Muhammad Idd Muhamad alipokuwa akiendesha kipindi chake cha ARRISALAH kinachorushwa Live na kituo cha Televishen cha Chanel Ten cha Jijini Dar es salaam.
"Jukumu la kuutukuza na kuuheshimu Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni letu sisi waislamu,ikitokea tukautukuza na tukauheshimu,itakuwa ni rahisi kwa wasiokuwa waislamu nao kuuheshimu mwezi huo,lakini sisi wenyewe tukiudharau basi hata wasio waislamu nao wataudharau"mwisho wa kumnukuu.
Sheikh Muhamadi Idd aliendelea kutanabaisha ya kwamba wapo walioruhusiwa kisheria kula mchana wa Ramadhan (ambapo aliwataja kuwa ni Wasafiri,Wagonjwa,Vikongwe,akina mama walioko katika Ada zao za mwezi) kwamba wale chakula hali ya kujistiri kwa maana wasile hadharani,lakini pia akina mama na akina dada wavae mavazi ya heshima.
Alitolea mfano kwamba sisi waislamu (na siyo wasio waislamu) ndiyo tuna utamaduni wa kutangaza na hatimaye kuvunja jungu kwa kufanya maasis mbalimbali ikiwemo kufanya uzinifu,ulevi na kuingia katika kumbi mbalimbali za starehe muda mfupi kabla ya kuanza mfungo wa Ramadhan,utaratibu huu ni haramu kwani hauwezi kuiaga haramu kwa kufanya haramu alikemea Sheikh Muhammad Idd.
Aidha aliwaomba masheikh,maimamu na waalimu wa madrasa ya kwamba waanze sasa kutoa elimu ya namna ya kufunga ikiwemo kuwajulisha mambo yanayo haribu swaumu, ili iwawezeshe waislamu kujuwa mambo muhimu yanayotakiwa kuyafanya muislamu ndani ya mwezi wa Ramadhan,kwani kuwapa mafunzo ya funga wakati tayari wapo ndani ya funga ni vizuri lakini si sahihi sana.
Sheikh Muhamad Idd aliyasema hayo alipokuwa akihudhurisha mada isemayo Mambo matano ya kuzingatia katika kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Sheikh Muhammad Idd Muhammad akiwasilisha mada Live kupitia kituo cha Luninga cha Chanel Ten jana usiku
0 comments:
Post a Comment