- Aliwahi kuwa mshauri wake.
Na mwandishi wetu kutoka zanzibar.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalimu Seif Sharif Hamad amefikwa na mtihani wa kufiwa na kaka yake akiyejulikana kwa jina la Ismail Sharif Hamad.
Msiba huo umetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni nyumbani kwa marehemu eneo la Mwanakwerekwe wilaya ya maghrib Zanzibar.
kwa mujibu wa mwakilishi wa blog ya munira aliyopo Zanzibar ambaye amezituma taarifa hizi jioni hii kwa njia ya mtandao,amesema marehemu alikuwa ana sumbuliwa na maradhi ya presha ambapo jana mara baada ya Al asri alizidiwa na kufariki dunia.
Mwakilishi wa blog ya munira akiongea na mmoja ya watu wa karibu wa mar hum huyo aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Rahman maarufu kwa jina la "mlala hoi alisema "marhum Ismail alikuwa mcheshi,akiongea na kila mtu zaidi ya yote,Mmungu alimpa kipaji cha busara iliyompelekea awe kimbilio la watu mbalmbali kutaka ushauri wake kwa mambo yao tofauti yakiyo wasibu,kwa kweli hili si pigo la familia pekee,bali ni pigo la wengi,mwisho wa kunukuu.
Kabla ya mwili wa mar hum kwenda kuzikwa katika makaburi ya mwanakwerekwe leo hii baada ya swala ya Adhuhuri,ilifanyika swala ya maiti katika Masjid Nnabawiyy uliopo mwanakwerekwe C eneo la nyumba mbili ambapo iliongozwa na
Msiba huo ulivuta hisia za watu wengi kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini,viongozi wa serikali na viongozi wa vyama vya siasa.ulihudhuriwa pia na makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd,mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Haruon Lipumba,Waziri wa Habari na Utamaduni (SMZ) mhe Said Ally Mbarouk,Wazir Muhameed Abuod na watu mbalimbali.
kwa mujibu wa makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,mar hum Ismail Sharif Hamad alizaliwa mwaka 1928,ameacha mjane,watoto na wajukuu,mwenyeezi mungu amrehemu na amsamehe makosa yake,aamiin.
Innaa lillaahi Wainnaa Ilayhi Rajiuun.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Hajj Khamis wakiwasili katika makaburi ya Mwanakwerekwe C kwa ajili ya kumuhifadhimar huum Ismail Sharif mapema leo hii.
Sehemu ya waumini wa kiislam waliohudhuria mazishi hayo.
Mwili wa Mar hum Ismail Sharif ukiingizwa ndani ya kaburi ikiwa ni sehemu ya mwanzo wa makazi yake mapya ya kuelekea Akhera.
Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba,akitia udongo katika kaburi la mar huum Ismail Sharif.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Hajj Khami,akitia udongo katika kaburi la mar huum Ismail Sharif.