UMOJA KWETU NI FARDHI-DOKTA SHEIN.
- HATUWEZI KUWA NA AMANI YA KWELI TUSIPOKUWA NA UMOJA WA KWELI.
- TUONDOSHE TOFAUTI ZETU.
Waislamu nchi na duniani kote wametakiwa kushikamana kwa dhati kwani kufanya hivyo ni wajibu kwetu.
Nasaha hizo zimetolewa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dokta Muhamad Shein katika hotuba yake iliyosoma kwa niaba yake na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Zanzibar Dakta Mwinyihaji Makame.
Akisoma hotuba hiyo ya ufunguzi wa Ijitimai liyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika msikiti wa Ole Kianga Pemba alisema,Mwenyeezi amefaradhisha umoja kwa waislamu,umoja ambao tukiwa nao kwa dhati ya imani yetu basi hakuna adui atakae tushinda zaidi ya kadari ya Mungu pekee.
Alionyesha masikitiko yake juu ya Waislamu kutokuwa na umoja wa kweli na kusababisha makundi yenye kutofautiana kwa mambo yasiyokuwa na wajibu kwetu.
Aidha alisema "hatuwezi kuwa na amani ya kweli pasipo kuwa na umoja wa kweli,kwani moja katika misingi ya amani ni watu kuwa na umoja wa kweli na pindi umoja ukikosekana na amani nayo inatoweka",hili la amani ni wajibu kwa kila mwanachi bila kujali itikadi yake ya dini au siasa na hata itikadi za kikabila alisisitiza mheshimiwa rais huku akitoa wito kwa waislamu kuongeza juhudi ya kutafuta elimu yadini na elimu ya mazingira.
Ijitimai hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Fii Sabili Llaah Markaz ya Zanzibar na kuhudhuriwa na Waislamu wengi kutoka ndani na nje ya nchi.
Moja kivutio katika Ijitimai hiyo alikuwa ni kijana Khamis Ali ambae ni kipofu aliehifadh juzuu 30 ambae alisoma Quran ya ufunguzi.
.
0 comments:
Post a Comment