Jamii ya kiislamu imetakiwa kuyafanyia kazi kivitenda juu ya elimu wanayoipata katika vituo mbalimbali vya elimu ikiwemo vituo vya madrasa.
Hayo yamesemwa katika hotuba ya makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya zanzibar mheshimiwa seif sharif hamad iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa habari,michezo,utamaduni na utalii wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar.
Amesema jamii ya kiislamu imekua ikilalamika juu ya kuporomoka kwa maadili hali ya kwamba wazazi wamesoma elimu ya dini kisha na wao kuwasomesha watoto wao lakini kwa kutoyafanyia kazi yale waliyoyasoma matekeo ya natija ya walichokisoma haionekana.
Hafla hiyo ya maulid ya kuzaliwa mtume s.a.w. iliyoambatana na sherehe za uzinduzi wa blog ya taasisi hiyo sambamba na uzinduzi wa kitabu cha "jifunze swala za faradhi kwa njia nyepesi" kilichotungwa na waandaaji wa hafla hiyo muniira madrasa taasisi iliyopo magomeni makuti.
0 comments:
Post a Comment