Jun 2, 2013

WAISLAMU WATAKIWA KUBADILIKA;

Wito umetolewa kwa waislamu kubadilika kwa mujibu wa nyakati na zama pasipo kuathiri imani na silka zao.

Wito huo umetolewa na mufti wa mombasa nchini kenya Sheikh Shaaban Abdi Mussa alipotoa mawaidha katika hafla ya uzinduzi wa blog ya taasisi ya muniira madrasa and islamic propagation Association  yenye makazi yake magomeni makuti.

Amesema tatizo kubwa walilonalo baadhi ya waislamu ni kuendelea na mazowea.

Alitolea mfano kwamba hata katika njia za ufundishaji bado baadhi yetu tunaendelea na mbinu za zamani kiasi kwamba mwalimu au sheikh hawezi kufundisha darsa hadi akae katika jamvi,wakati zama tulizonazo haziendani na nyenzo hizo.

Lakini pia amesema zama hizi mafundisho yanatolewa kupitia projector au kwa njia za lap top lakini bado baadhi yetu hatujawa na fikra za kutumia njia hizo.

Aidha alisema wakati umefika tuwaandae watoto wetu kuzitumikia fani mbalimbali zikiwemo za uandisi,udaktari na kadhalika.

Alitolea mfano kwamba hata mtume s.a.w aliandaliwa kwenda kuonana na mungu katika safari yake ya miiraji na israa.

"mtume alipasuliwa kifua chake na kutolewa uchafu muda mfupi kabla ya kwenda israa",hii ni ishara ya kwamba mtume aliandaliwa akakutane na mola wake,alisema Sheikh Shaaban.

 Mufti wa mombasa nchini kenya sheikh Shaaban Abdi mussa akitoa waadhi kwa waumini waliofurika katika hadhara ya uzinduzi wa blog ya taasisi ya MuniiraMadrasa na uzinduzi wa kitabu cha Jifunze Swala za Faradhi kwa njia nyepesi,kulia kwake ni katibu mkuu wa taasisi hiyo Ustaadh Juma Rashid,anaye fuatia ni Waziri wa Habari michezo,utamaduni na utalii wa serikali ya zanzibar Mhe Said Ally Mbaruok,anayefuatia ni sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Al had Mussa Salum na wa mwisho ni mnadhimu wa Vyombo vya habari vya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambaye pia ni amiri wa vyombo vya habari vya kiislam Tanzania Maalim Juma Mmanga.

0 comments:

Post a Comment