Mar 21, 2016

ULINZI MKALI WAIMARISHWA KABLA YA KUTANGAZA MATOKEO ZANZIBAR.

Wafuasi wa upinzani walikusanyika nje ya makao makuu ya CUF Zanzibar tarehe 28 Oktoba, baada ya kutangazwa kuwa uchaguzi umefutwa.
Wafuasi wa upinzani walikusanyika nje ya makao makuu ya CUF Zanzibar tarehe 28 Oktoba, baada ya kutangazwa kuwa uchaguzi umefutwa.

Baada ya uchaguzi mkuu wa marudio kufanyika Jumapili hii Machi 20, vikosi vya usalama na jeshi vimeimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, wakati ambapo kukisubiriwa kutangazwa matokeo ya uchaguzi.

Mbwa walinzi wamepelekwa katika eneo ambako matokeo hayo yatatangazwa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Selim Jecha Selim anatazamiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo mkuu wa marudio.

Uchaguzi mkuu wa marudio umefanyika Jumapili hii, baada ya tume ya Uchaguzi kisiwani Zanzibar kufuta uchagizi wa awali ikidai kwamba ulikua uligubikwa na udanganyifu mkubwa. Jambo ambalo lilikosolewa na Marekani , baaadhi ya nchi za Ulaya na Afrika.

Lakini mpaka sasa Tume ya Uchaguzi bado haijasema ni saa ngapi matokeo ya kwanza yataanza kutangazwa, licha ya vyanzo kutoka Tume hiyo kubaini kwamba huenda zoezi hili likaanza mchana.

Chama cha CUF, ambacho kilisusia uchaguzi huu na kuwataka wafuasi wake wasusie uchaguzi ambao kiliutaja si halali, bado kilikua kwenye orodha ya vyama viliyoshioriki katika uchaguzi uliofanyika Jumapili hii

Kiwango cha ushiriki katika uchaguzi huo kilikua kidogo.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar watu 503,860 ndio walijiandikisha kupiga kura.


Pia kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Wagombe kumi na nne ndio wameshirikishwa katika uchaguzi wa jana. 
Wagombea hao ni pamoja na Khamis Iddi Lila wa chama cha ACT-W, Juma Ali Khatib wa ADA-TADEA, Hamad Rashid Mohamed wa ADC, Said Soud Said wa AFP, Ali Khatib Ali wa CCK, Ali Mohamed Shein wa CCM, Mohammed Massoud Rashid wa CHAUMMA, Seif Sharif Hamad wa CUF, Taibu Mussa Juma wa DM, Abdalla Kombo Khamis wa DP, Kassim Bakar Aly wa JAHAZI, Seif Ali Iddi wa NRA, Issa Mohammed Zonga wa SAU, Hafidh Hassan Suleiman wa TLP.

0 comments:

Post a Comment