Feb 21, 2015

KUTOWAAJIRI WAKHITIMU WA MAFUNZO YA KIJESHI,NI KUZALISHA MAJAMBAZI

 

 MHESHIMIWA MAGDALENA SAKAYA,MBUNGE WA VITI MAALUMU NA NAIBU KATIBU MKUU CUF TANZANIA BARA.

Serikali imelaumiwa kwa kua ni chanzo cha kuzalisha majambazi hapa nchini.

Lawama hizo zimetolewa leo jioni na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi Mhe Magdalena Sakaya alipokua anawahutubia Wananchi wa Kata ya Makumbusho iliyopo Mwananyamala Jijini Dar esalaam.

Amesema vijana wengi wanakubali kujiunga na mafunzo ya kijeshi wakiamini wakisha hitimu watapata ajira,lakini hali inakua ni kinyume cha hivyo.

"Tuna shuhudia vijana wengi baada ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi wanakosa ajira,matokeo yake kwa kua mafunzo wanayo na hawana kazi ndipo baadhi yao wanajiingiza katika ujambazi", alisema.

"Kwa hili,Serikali wanabeba lawama,kwani Ujambazi huu,wao ndiyo wanaouzalisha" , mwisho wa kumnukuu.

Wakati huo huo,Mhe Sakaya ameitilia shaka sera ya elimu iliyozinduliwa hivi karibuni na Mhe Rais Jakaya Kikwete kwa madai ni sera isiyotekelezeka.

"Ndugu wananchi,kabla ya kuzinduliwa sera hii,sera ya elimu ilikua inawataka watoto yatima na masikini (wasiojiweza) wasome elimu ya msingi bure,lakini sera hiyo haijatekelezwa na watoto hao walisimamishwa masomo na kukosa elimu,leo elimu iwe bure kwa ngazi ya msingi na elimu ya kati,haya ni mashaka" ,mwisho wa kumnukuu.


0 comments:

Post a Comment