Utata umezingira suala la kijana George Mgoba, ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa kiongozi wa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) baada ya habari kuwa alitekwa na baadaye kutupwa kwenye Msitu wa Pugu, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Si Jeshi la Polisi mkoani Pwani wala Dar es Salaam
lililokuwa tayari kuzungumzia tukio la kijana huyo kutekwa, kupigwa na
kutekelezwa kwenye msitu huo, lakini msemaji wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MHN) alithibitisha kuwapo kwa kijana huyo hospitalini hapo
kuanzia jana saa 10:30 jioni, ingawa hakutaka kutoa maelezo mengi.
Mgoba amekuwa akihamasisha vijana wenzake
waliohitimu ya JKT kukusanyika jijini Dar es Salaam na kuandamana hadi
kwa Rais ili kumweleza masikitiko yao ya kutopatiwa ajira baada ya
kumaliza mafunzo kama walivyoahidiwa wakati wakienda kwenye kambi za
jeshi hilo.
“Ndio aliletwa hapa majira ya saa 10:30 akitokea Hospitali ya Amana,” alisema ofisa uhusiano wa MHN, Aminiel Aligaeshi.
“Lakini waganga walipotaka kumtibu alikataa kwa
sharti kwamba atibiwe wakati ndugu zake wakiwapo.
Ndugu zake walipofuatwa nje, hawakuonekana. Anaonekana ana maumivu sehemu ya mgongoni na anapumua kwa shida.”
Ndugu zake walipofuatwa nje, hawakuonekana. Anaonekana ana maumivu sehemu ya mgongoni na anapumua kwa shida.”
Habari zinasema kuwa kuanzia saa 1:00 jioni
madaktari walikuwa wakijaribu kumshauri akubali kutibiwa, lakini
akakataa na hivyo kuwalazimu madaktari kumtaka asaini fomu ya kukataa
matibabu.
Hata hivyo hadi saa 2:00 usiku hakuwa amesaini.
Hata hivyo hadi saa 2:00 usiku hakuwa amesaini.
Kijana huyo anasemekana kutekwa juzi jioni na watu
ambao hawajajulikana na aliokotwa na msamaria mwema ambaye baadaye
aliungana na watu wengine kumpeleka Hospitali ya Tumbi.
Hata hivyo, aligoma kutibiwa kwenye hospitali hiyo akitaka ndugu zake wawepo.
Habari zinasema baadaye alisafirishwa kuhamishiwa
Hospitali ya Amana kabla ya kuhamishwa tena na kwenda Muhimbili jana saa
9:00 alasiri.
Mfanyakazi mmoja wa Hospitali ya Amana aliiambia
gazeti hili kuwa kabla ya askari wa Jeshi la Polisi kumfuata na gari
mbili aina ya Land Rover, kundi la vijana wanaosadikiwa kuwa ni wahitimu
wa mafunzo ya JKT, liliwasili Amana na kutaka kushinikiza kumchukua
Mgoba, lakini uongozi uliwakatalia kwa maelezo kuwa wangetoa ruhusa hiyo
kama wangekuwapo ndugu zake.
Alivyotekwa
Mwandishi wetu kutoka Kibaha anaripoti kuwa kijana
huyo, anayejielezea kuwa ni mtetezi wa vijana waliohitimu JKT,
aliokotwa kwenye kichaka kilichopo Picha ya Ndege mjini humo akiwa
amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwilini.
0 comments:
Post a Comment