Wananchi wa Palestina wa ardhi
zilizoanza kukaliwa kwa mabavu mwaka 1948 na kupewa jina la Israel
wamelaani kitendo cha gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot cha
kuchapisha katuni zinazoitusi na kuivunjia heshima shakhsia tukufu ya
Bwana Mtume Muhammad SAW.
Vyama vya Waarabu katika ardhi za Palestina
zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni tangu mwaka 1948 leo vimetoa taarifa
ya pamoja, ambapo mbali na kulaani kitendo cha gazeti la Kizayuni la
Yediot Ahronot cha kuchapisha vikatuni vya kumkejeli na kumvunjia
heshima Bwana Mtume SAW vimeeleza kuwa lengo la hatua hiyo, bila ya
shaka yoyote ni kuchochea hisia za Waislamu.
Hapo kabla pia magazeti ya
utawala wa Kizayuni wa Israel yaliwahi kuchukua hatua za kumvunjia
heshima Bwana Mtume Muhammad SAW…/
0 comments:
Post a Comment