Feb 4, 2015

16 wauawa katika machafuko yanayoendelea Libya

Kwa uchache wanajeshi 16 wa Libya wameuawa na wengine 38 kujeruhiwa kufuatia mapigano tofauti yaliyotokea kando kando ya ngome ya waasi mashariki mwa nchi hiyo.
Ripoti zinasema kuwa, kwa akali jeshi la Libya limepoteza wanajeshi wake 11 baada ya kuanzisha mashambulio dhidi ya wabeba silaha katika mji wa Derna. 

Kanali Ahmed al-Mashari mmoja wa makamanda wa jeshi la nchi hiyo amesema kuwa, makundi ya wabeba silaha yamepata hasara kubwa katika mapigano hayo. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh linaloendesha operesheni za kigaidi nchini Iraq na Syria wameingia nchini Libya. 

Libya imeendelea kushuhudia hali ya mchafukoge na mauaji tangu ulipong'olewa madarakani utawala wa Kanali Muammar Gaddafi, chini ya uungaji mkono wa Jumuiya ya NATO, kiasi cha kupelekea taifa hilo la kaskazini mwa Afrika kuongozwa na serikali mbili na mabunge mawili, huku moja ikiwa haitambuliwi kimataifa.

0 comments:

Post a Comment