Jan 19, 2015

Taarifa muhimu kwa Waislamu

MNAWEZA ISOMA VIZURI HII.          Leo kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 11 jioni tulikuwa ktk ukumbi Wa Julius Nyerere Conference  katika kikao cha kamati ya  GB sheria na katiba tukiwawasilisha mapendekezo ya muswada Wa mahakama ya kadhi.

Tulikuwa taasisi 11 ambazo ni baraza kuu la jumuiya na taasisi za kiislamu Tanzania,  Annahar, Basuta, Tampro, Dumt, Shura ya maimamu, jumuiya na taasisi nk nkwa upande mmoja na bakwata upande wa pili, TLS, nk.

 Pia alialikwa Jaji Robert Makaramba na Arcado Ntagazwa. Maoni ya Jaji Robert makaramba ni kuwa mahakama ya kadhi ni chombo halali na hakipaswi kuitwa cha kidini bali ni chombo cha dola, kigharamiwe na dola.

Alisema wakristo wasilalamike sababu hata mahakama za kawaida zinatumia sheria za kikristo ambazo zinatokana na common law.

Kwa upande mwingine maoni ya bakwata wao wameiambia kamati ya binge kuwa kadhi koti  ni mahakama ya kidini hivyo isigaramiwe na dola bali zijigharamie zenyewe.

Wakihalalisha hoja zao bakwata walitoa mfano kua kama  tunavyogharamia Maji ya udhu mikeka na umeme misikitini.

 Aidha walienda kudai kwamba mahakama ya kadhi hiyo ndio hii mufti aliyoiunda, na kwamba muft anayetajwa na muswada awe ni mufti Wa bakwata hiyo iwe rasmi ndani ya sheria.

Kwa upande wao TLS  wanapendekeza muswada huu uondolewe haufai.

Maoni ya bakwata yamewasilishwa na Katibu Wa bakwata Mzee lolira na sheikh Jongo.

Wakati maoni ya Maoni yetu ya Taasisi 11kama yalivyoandaliwa na wanasheria kwa ushirikiano na masheikh yamewasilishwa na wakili Yahya Njama.

Kimsingi tumesema huu muswada haufai uondolewe na badala yake kamati tumeiomba ipokee ,muswada mbadala tuliouandaa ambao unaunda kadhi court, unaunda bodi ya Islamic law ambayo ndio itakayoteua makadhi na kudhibiti nidhamu za makadhi,alisema mpashaji wetu.

Aliendelea kutosha kwamba Waziri asipewe mamlaka ya kutunga sheria au kanuni zinazohusu waislamu bila ya kushauriana na wanazuoni, mahakama ya kadhi tumetaka iwe sehemu ya judiciary, igharamiwe na dola, bakwata na mufti wasiwe ndio wateuzi Wa makadhi.

 Na pia tumeitaka kamati ya binge iishauri serikali iuondoe muswada wake haufai na wala haukidhi vigezo vya kuunda chombo chenye hadhi ya mahakama.

Bwana Ntagazwa ameeleza historia ya kadhi court na ameeleza kuwa muswada huu hauna nia ya dhati kuanzisha kadhi court ya ukweli bali nia ni kupata kura za waislamu tu, aliungana nasi kuwa muswada uondolewe

Na TLS CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA nao waliunga mkono
hoja zetu kwa kiasi kikubwa.

Ktk kikao hicho Kwa upande wetu tulikuwa  Mimi , walii Njama, Dr Benhajj wakili hamza Jabir masheikh Kundecha Kilemile sheikh bawazir sheikh mbalamwezi mwana historia Mohamed said na
wengi wengine. Alhamdulillah tuliwakilisha vyema na wrote walituelewa tunaamini kazi tuliitimiza yaliyobaki Allah anajua zaidi.

Mjadala ulikuwa mkali kutwa
nzima lakini tuliwatuliza

0 comments:

Post a Comment