Jan 18, 2015

Balozi wa Ufaransa atimuliwa kwenye kikao Sudan

Balozi wa Ufaransa nchini Sudan, Bruno Aubert ametimuliwa kwenye kikao cha waandishi wa habari mjini Khartoum nchini humo.
Bruno alitimuliwa na waandishi wa habari kufuatia kitendo cha jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo kuchapisha tena picha za vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu (saw). 

Wakuu wa kituo cha habari cha Twayyibah Press, ambao walikuwa wameandaa mkutano huo, walishangazwa kuhudhuria balozi huyo bila ya kualikwa. 

Ripoti hiyo imesema kuwa, balozi huyo wa Ufaransa alitaka kuzungumza katika kikao hicho kupitia nafasi ya mtaalamu mmoja wa masuala ya ustawi wa utamaduni ambaye ni raia wa Ufaransa, lakini akajikuta akifukuzwa na waandishi hao huku wakimwambia kuwa hiyo haikuwa nafasi yake. 

Baadaye waandaaji wa kituo hicho cha Twayyibah waliwaambia waandishi wa habari kuwa, waliamua kuchukua hatua hiyo kulaani kitendo cha gazeti la Charlie Hebdo kwa kuchapisha picha za vikatuni vinavyomvunjia heshima Bwana Mtume Mtukufu wa Uislamu (saw).

0 comments:

Post a Comment