Nov 26, 2014

Mapigano kati ya mashabiki wa mpira na polisi DRC

Mapigano mapya yameibuka kati ya polisi na mashabiki wa mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupelekea watu kadhaa kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mapigano hayo yamejiri katika mji wa pili kwa ukubwa wa Lubumbashi, kusini mashariki mwa nchi hiyo na kwamba, machafuko hayo yaliibuka baada ya kumalizika mchuano wa mpira kati ya timu mbili hasimu mjini humo. 

Duru za kidaktari zimesema kuwa, watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine kadhaa wakipoteza maisha katika mapigano kati ya mashabiki hao na polisi. Aidha watu wengine wamejeruhiwa katika tafrani hizo. Mashuhuda wanasema kuwa, mapigano yaliibuka kufuatia mwamuzi kukataa goli la timu ya mji wa Lubumbashi na kupelekea mechi kumalizika kwa sare kati ya timu mbili. 

Jean-Oscar Sangusa Mutunda, Meya wa mji wa Lubumbashi amesema kuwa, polisi waliwashambulia mashabiki ambao walikuwa na hasira kufuatia kukataliwa goli la timu ya mji wao. 

Tayari wakuu wa vyombo vya mahakama, wameahidi kuanzisha uchunguzi wa tukio hilo na sheria kuchukua mkondo wake dhidi ya wahusika.

0 comments:

Post a Comment