Sep 3, 2014

Nyani awagawia watu pesa India


Nyani hawa aina ya Macaque huabudiwa na watu nchini India

Nyani mmoja katika jimbo la Himachal Pradesh Kaskazini ya India, amewagawia watu pesa taslimu kutoka mtini.

Taarifa zinasema kuwa watu waliokuwa wanajivinjari katika mji wa Shimla jimboni humo, walianza kukimbia huku na kule wakiokota pesa zilizokuwa zinarushwa na Nyani huyo kutoka juu ya mti kwa karibu saa moja.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa Nyani huyo kwa jina Simian aliiba pesa hizo Rupee 10,000 kutoka kwa nyumba ya jirani katika eneo hilo.

Nyani huyo aliingia katika nyumba hiyo kutafuta chakula lakini alipokosa chakula akaamua kutoweka na pesa.

Kuna karibu Nyani 300,000 katika eneo hilo. Jimbo la Shumla limekuwa makao kwa wanyama wengi.

Nyani aina ya Macaque, huonekana kama wanyama wa kuabudiwa na hivyo hulishwa na wakazi.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanyama hao, wamekuwa wakizozana na wakazi kwa sababu ya kuharibu mimema , kushambulia watu na hata kuwauma watoto.

Maafisa tayari wametangaza wanyama hao kuwa kero kubwa kwa wakazi.

Nyani huyo mwanzo alionekana akiwa ameketi juu ya paa la nyumba akiwa na bunda la noti kabla ya kuanza kuwagawia watu pesa hizo kwa kuwarushia.

watu walipoanza kukusanya pesa hizo, Nyani huyo alikimbilia kwenye mti mwingine.Lakini watu waliokuwa wanokota pesa hizo walimfuata kwani pesa haziachiki.

"Nyani alionekana kushutushwa na idadi ya watu waliokuwa wanamfuata lakini alipokimbilia kwenye mti mwingine, watu waliendelea kumfuata,'' alisema mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment