Sep 2, 2014

Amnesty International yaonya hali Iraq


Jamii ya walio wachache, Iraq

Shirika la Amnesty International limesema kuna kampeni ya kumaliza jamii ya wachache Iraq.
 
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema lina ushahidi kwamba waasi wa Islamic State wanatekeleza kile walichokiita kampeni ya kumaliza jamii ya wachahe kaskazini mwa Iraq.
Taarifa zinasema kwamba wapiganaji hao wa kundi la Islamic State wametenda kosa la jinai, ikiwemo kutekeleza mauaji ya watu wengi na utekaji nyara dhidi ya kabila la walio wachache nchini humo.

Amnesty International imesema kwamba mauaji ya watu wengi yamefanyika mwezi uliopita wa Nane katika jimbo la Sinjar na kusababisha mamia ya watu wa jamii ya Yazid kuuawa.


Duncan Spinner ambaye anaongoza Tume ya Kimataifa inayohusika na upoteaji wa watu katika maeneo yenye migogoro kwa upande wa Iraq, amesema wameagizwa na serikali ya nchi hiyo kufanyia uchunguzi makaburi yanayohisiwa kuzikwa watu wengi, iwapo hali ya usalama itaruhusu. 


Katika hatua nyingine Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imekubali kutuma timu nchini Iraq kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na wapiganaji hao wa kislamu.

Tume hiyo imesema inaushahidi wa kutosha kuhusiana na uhalifu huo wa kivita.
Umoja wa Mataifa umesema Zaidi ya watu elfu moja wengi wao wakiwa raia wameuawa mwezi uliopita.

0 comments:

Post a Comment